Sisi ni nani

Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) ni Wakala chini ya Wizara ya Ujenzi ulioanzishwa chini ya mamlaka ya sheria ya wakala za serikali Na. 30 ya mwaka 1997 kwa amri ya serikali na Waziri wa Ujenzi kupitia tangazo la serikali Na. 254 la tarehe 26 Agosti 2005,kuchukua majukumu ambayo hapo awali yalifanywa na Kitengo cha Umeme na Mitambo (E&M) cha Idara chini ya Wizara ya Ujenzi iliyokuwa na ari ya kuboresha huduma na kuongeza tija na ufanisi. TEMESA ilianzishwa mahususi kutoa huduma za Umeme, Mitambo na Elektroniki, Huduma za vivuko pamoja na Ukodishaji Mitambo kwa taasisi za serikali na Umma kwa jumla.