Kazi za Kitengo cha Usimamizi wa Ununuzi
Kutoa utaalamu na huduma katika ununuzi, uhifadhi na usambazaji wa bidhaa na huduma kwa Wakala.
Kitengo hiki kitafanya kazi zifuatazo:
(i) Kutumikia kama katibu wa Bodi ya Zabuni.
(ii) Kuandaa na kuhuisha Mpango wa Ununuzi wa mwaka kwa ununuzi wa bidhaa, kazi, huduma zisizo za ushauri na huduma za ushauri.
(iii) Kuandaa taarifa za kila mwezi zinazotumika kwa utekelezaji wa mpango wa ununuzi wa Bodi ya Zabuni, menejiment, idara na washika dau wengine.
(iv) Kuhakikisha taratibu na mchakato wa manunuzi unazingatiwa kulingana na Sheria ya Ununuzi wa Umma na kanuni zake.
(v) Kufanya manunuzi, kudumisha na kusimamia ununuzi wa vifaa na huduma kwa kuzingatia ubora wa bidhaa na thamani ya fedha.
(vi) Kuhakikisha vifaa vya ofisi vinatunzwa na kuhifadhiwa kwa usahihi, vinasambazwa kwa wakati na kuwafikia wahusika kwa wakati.
(vii) Kutoa ushauri wa kiufundi kwa menejimenti, Bodi ya Zabuni, idara husika na wadau wengine juu ya masuala yanayohusu shughuli za ununuzi kwa kufuata, kanuni na taratibu za ununuzi.
(viii) Kuwa kama kiungo kati ya Wakala na PPRA juu ya masuala yanayohusu ununuzi.
(ix) Kuandaa hati za zabuni kwa ununuzi wa bidhaa, kazi, huduma za ushauri na mali kama ilivyo kwa kanuni.
(x) Kusaidia usimamizi wa mikataba/ kandarasi na utawala, pamoja na Uratibu wa mikataba na vile vile utoaji wa mikataba iliyoidhinishwa.
(xi) Kuandaa na kutunza rejista ya mali za Wakala.