HOTUBA YA WAZIRI WA UJENZI MHESHIMIWA ABDALLAH ULEGA AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2025/2026
Imewekwa Monday 5th May , 2025
HOTUBA YA WAZIRI WA UJENZI MHESHIMIWA ABDALLAH HAMIS ULEGA (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA
MWAKA WA FEDHA 2025/2026
|
Dira
Kuwa na miundombinu bora na endelevu itakayochochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.
Dhima
Kusimamia ubora, uhakika na usalama wa kazi za ujenzi wa barabara, madaraja, vivuko, majengo, mitambo, umeme na vifaa vya kielektroniki kwa kushirikiana na wadau kwa maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii yanayokidhi mahitaji ya wananchi.
Majukumu
- i.Kusimamia Utekelezaji wa Sera ya Ujenzi;
- ii.Kusimamia Ujenzi na Ukarabati wa Barabara na Madaraja;
- iii.Kusimamia Ujenzi na Usimamizi wa Vivuko;
- iv.Kusimamia Shughuli za Ufundi na Umeme;
- v.Kusimamia Ujenzi na Usimamizi wa Majengo ya Serikali;
- vi.Kusimamia Makandarasi na fani za Wahandisi, Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi;
- vii.Kuandaa muundo wa madereva wa Serikali;
- viii.KusimamiaMaendeleoyaWatumishikatika Wizara; na
- ix.Kusimamia Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi (TANROADS, TEMESA, TBA, ICoT, NCC,
Vikosi vya Ujenzi, RFB, AQRB, CRB na ERB).
A.UTANGULIZI
- 1.Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa hapa Bungeni na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu iliyochambua utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Ujenzi ya mwaka wa fedha 2024/25, ninaomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako Tukufu sasa likubali kupokea na kujadili Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2024/25. Aidha, ninaliomba Bunge lako Tukufu liridhie kupitisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2025/26.
- 2.Mheshimiwa Spika, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, kwa kutujaalia afya njema na kutuwezesha kukutana leo hii hapa Bungeni.
- 3.Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii adhimu, na kwa unyenyekevu mkubwa, kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuendelea kuniamini, na kuniteua kuwa Waziri wa Ujenzi tangu tarehe 08 Desemba, 2024. Naomba kupitia kwako nimuahidi Mheshimiwa Rais kuwa, kwa kushirikiana na watendaji wenzangu katika Wizara, nitatekeleza majukumu haya niliyopewa kwa uaminifu na moyo wa uzalendo.
- 4.Mheshimiwa Spika, sambamba na shukrani hizo kwa Mheshimiwa Rais, kipekee nitumie fursa hii kumpongeza kwa kazi kubwa ambayo anaendelea kuifanya ya kuliongoza Taifa letu. Sote ni mashuhuda wa namna alivyofanya mapinduzi makubwa katika sekta zote nchini. Chini ya uongozi wake tumeshuhudia
miradi mikubwa, katika sekta mbalimbali ikiwa ni pamoja na sekta ya ujenzi inavyoendelea kutekelezwa nchi nzima. Kukamilika kwa miradi hii kunachochea maendeleo ya sekta nyingine za kiuchumi na kijamii na hivyo kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. Hakika Watanzania tunajivunia na tunatembea kifua mbele chini ya uongozi imara wa Mheshimiwa Rais.
- 5.Mheshimiwa Spika, naomba kuwapongeza Mheshimiwa Dkt. Philip Isdory Mpango, Makamu wa Rais; Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu na Mheshimiwa Dkt. Doto Mashaka Biteko (Mb.), Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumsaidia na kumshauri vyema Mheshimiwa Rais katika uongozi wa nchi yetu. Viongozi hawa pia wamekuwa wakitoa miongozo na maelekezo mbalimbali ambayo yamesaidia sana katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Ujenzi. Nawashukuru sana.
- 6.Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii pia kukupongeza wewe binafsi pamoja na Naibu Spika kwa namna mnavyoongoza kwa weledi Bunge hili la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambalo litafikia tamati katika Mkutano huu. Aidha, nitumie nafasi hii kutoa shukrani kwa Ofisi yako, Katibu wa Bunge na watendaji wa Ofisi ya Bunge kwa ushirikiano ambao mmetupatia wakati wote katika utekelezaji wa majukumu yetu.
- 7.Mheshimiwa Spika, kipekee napenda kuishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu chini ya uongozi wa Mwenyekiti, Mheshimiwa Selemani Moshi Kakoso (Mb.) na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Anne Kilango Malecela (Mb.). Kamati hii imekuwa bega
kwa bega na Wizara katika utekelezaji wa majukumu yake kupitia maelekezo, maoni na ushauri katika masuala mbalimbali. Hali kadhalika, Kamati hii ilifanya uchambuzi wa kina wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2024/25 na kutoa ushauri ambao umezingatiwa katika bajeti hii ninayoisoma mbele ya Bunge lako.
- 8.Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii pia kutoa mkono wa pole kwako wewe binafsi, Mheshimiwa Spika, Bunge lako, Chama cha Mapinduzi, wananchi wa Jimbo la Kigamboni, marafiki na familia, kufuatia kifo cha Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigamboni. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
- 9.Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 16 Novemba, 2024, yalitokea maafa makubwa kutokana na kuporomoka kwa jengo la ghorofa nne katika eneo la Kariakoo Jijini Dar es Salaam. Ajali hiyo ilisababisha vifo, majeruhi pamoja na upotevu wa mali. Nitumie nafasi hii kutoa pole kwa wote walioathirika na maafa haya, na ninawaombea marehemu wote wapumzike kwa amani. Wizara yangu, ikiwa ni msimamizi wa shughuli za majenzi nchini, inaendelea na taratibu za kutunga Sheria ya Majengo kwa ajili ya kusimamia Sekta ndogo ya Majengo nchini. Sheria hii itakapoanza kutumika itakuwa muarobaini wa changamoto zilizopo hususan katika masuala ya uratibu, usimamizi na udhibiti wa sekta hiyo hapa nchini.
- 10.Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kwa mara nyingine kutoa pole kwa wananchi kutokana na adha iliyotokea baada ya daraja la dharura la Somanga- Mtamakukatikanakusababishachangamotoya
mawasiliano baina ya mkoa wa Pwani na Mikoa ya Kusini. Daraja hili lipo katika eneo linapojengwa daraja jipya la kudumu katika mpango wa matengenezo yanayoendelea kufuatia uharibifu uliotokea mwaka jana kutokana na mvua za El-nino na Kimbunga Hidaya. Aidha, nitoe pole kwa wananchi katika maeneo mengine nchini yaliyoathirika kutokana na uharibifu wa miundombinu ya barabara na madaraja. Niwaondoe hofu na kuwapa matumaini wananchi kuwa Serikali, chini ya Mheshimiwa Rais, Daktari Samia Suluhu Hassan ipo kazini mchana na usiku ili kurejesha mawasiliano katika hali yake ya kawaida kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
- 11.Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo ya utangulizi, niruhusu sasa nitoe taarifa ya Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2024/25 pamoja na Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2025/26. Aidha, kabla ya hayo, naomba nitoe taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020.
B.MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA MALENGO YALIYOAINISHWA KATIKA ILANI YA CCM YA MWAKA 2020
- 12.Mheshimiwa Spika, mwaka huu ni wa kipekee kwani nchi yetu itafanya uchaguzi mkuu wa kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani. Tunapoelekea katika uchaguzi huo, ni vyema tutoe taswira ya jumla ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020 ambayo iliaminiwa na wananchi hadi kuipa CCM dhamana ya kuongoza nchi kwa kipindi cha mwaka 2020hadi2025.Nitumiefursahiikwamuhtasari
kutoa taarifa ya utekelezaji wa Ilani hiyo kwa masuala yanayohusu Wizara ya Ujenzi yaliyopo katika Ibara 55 (a-b) – Masuala ya Kisera; 55 (c-g) - Barabara na Madaraja na Usalama Barabarani; 55 (h) – Nyumba na Majengo ya Serikali; 57 (j) – Vivuko na 59 (h) – Viwanja vya Ndege.
- 13.Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa masuala haya ni kama ifuatavyo:
a. Kuimarisha Mfuko wa Barabara
- 14.Mheshimiwa Spika, Mfuko wa Barabara ulianzishwa mwaka 2000, mahsusi kwa ajili ya kugharamia matengenezo ya barabara nchini. Serikali imefanikiwa kuongeza makusanyo ya Mfuko wa Barabara kutoka Shilingi bilioni 899.2 mwaka 2020/21 hadi Shilingi bilioni 1,113.3 mwaka wa fedha 2023/24 sawa na ongezeko la asilimia 24. Aidha, hadi Aprili, 2025, makusanyo ya fedha za Mfuko kwa mwaka wa fedha 2024/25 yalikuwa yamefikia Shilingi bilioni 905.2. Ongezeko hili limewezesha kuimarika kwa uwezo wa Mfuko kugharamia matengenezo ya barabara nchini.
b. Kuunganisha makao makuu ya mikoa na nchi jirani kwa barabara za lami
- 15.MheshimiwaSpika,Wizara imeendelea kujenga barabara za lami za kuunganisha makao makuu ya mikoa na nchi jirani. Miradi iliyokamilika katika kipindi hikini kuunganisha mikoa ifuatayo:
- i.Tabora na Singida kupitia barabara ya Chaya – Nyahua (km 85.4);
- ii.Tabora na Katavi kupitia barabara ya Tabora – Koga – Mpanda (km 342.9); na
- iii.Kigoma na Kagera kupitia barabara ya Kabingo – Kasulu – Manyovu (km 260.6).
Vilevile, miradi mbalimbali ya barabara za kuunganisha nchi yetu na nchi jirani imetekelezwa katika kipindi cha miaka mitano. Miradi iliyokamilika ni kuunganisha Tanzania na nchi zifuatazo:
- i.Tanzania na Malawi kupitia barabara za Mpemba – Isongole (km 50.3) na Mbinga – Mbambabay (km 66) ambazo zimekamilika; na
- ii.Tanzania na DRC kupitia barabara ya Sumbawanga – Matai – Kasanga Port (km 107).
- 16.Mheshimiwa Spika, aidha, Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi ya barabara mbalimbali za kuunganisha mikoa ambayo haijaunganishwa kwa barabara za kiwango cha lami kama ifuatavyo:
- i.Rukwa na Katavi; ujenzi wa sehemu ya Kibaoni – Sitalike (km 50) unaendelea;
- ii.Katavi na Kigoma; ujenzi wa sehemu ya Vikonge – Mishamo Jct (km 62.7) unaendelea;
- iii.Kigoma na Tabora; ujenzi wa sehemu ya Uvinza – Malagarasi (km 51.1) unaendelea;
- iv.Singida na Mbeya; ujenzi wa sehemu ya Mlongoji – Itigi – Mkiwa (km 56.9) unaendelea;
- v.Morogoro na Njombe; sehemu ya Ifakara – Mbingu – Chita (km 100) ujenzi unaendelea;
- vi.Morogoro na Ruvuma; ujenzi wa sehemu ya Ifakara – Lupiro – Mtimbira (km 112) Mkandarasi yupo katika hatua za awali za kuanza ujenzi;
- vii.Tanga na Manyara; Ujenzi wa sehemu ya Handeni – Mafuleta – Kileguru (km 50) unaendelea. Mkandarasi wa sehemu ya Handeni – Kang’ata (km 30) yupo katika hatua za awali za kuanza ujenzi;
- viii.Arusha na Mara; ujenzi wa sehemu ya Waso – Sale (km 49) umekamilika na ujenzi wa sehemu ya Natta – Sanzate unaendelea;
- ix.Arusha na Shinyanga; Mkandarasi wa sehemu ya Nkoma – Lalago (km 65) yupo katika hatua za awali za kuanza ujenzi; na
- x.Njombe na Mbeya; ujenzi wa sehemu ya Njombe – Makete (km 107) umekamilika na ujenzi wa sehemu ya Kitulo – Iniho (km 36.3) unaendelea.
c.Kushirikisha kikamilifu vikundi vya wananchi pamoja na Makandarasi wadogo katika kazi za matengenezo ya barabara
- 17.Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TANROADS imekuwa ikitoa kazi za matengenezo ya barabara zisizotumia mitambo (Labour based methods) kupitia mikataba na Makandarasi wadogo au nguvu kazi ya ndani ya Wakala (Force account). Kupitia mikataba hii, TANROADS hutekeleza shughuli za matengenezo kwa kutumia vifaa na/au vibarua kutoka katika maeneo ya
miradi.
d.Kuendelea kuwajengea uwezo Makandarasi wazalendo ili kushiriki kikamilifu kwenye kazi kubwa za ujenzi
- 18.Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kutoa vipaumbele kwa Makandarasi wazawa kwa zabuni zote za ujenzi na matengenezo ya barabara zinazoendelea hapa nchini. Serikali kupitia Sheria ya Ununuzi wa Umma, (Sura ya 410) na kanuni zake za mwaka 2024 inaekeleza miradi yote yenye thamani chini ya Shilingi billioni 50 itekelezwe na Makandarasi wazawa. Jumla ya mikataba 5,264 ya matengenezo ya barabara yenye thamani ya kiasi cha Shilingi trilioni 1.963 ilisainiwa na kutekelezwa na makandarasi wazawa. Aidha, TANROADS inaendelea na taratibu za ununuzi kwa Makandarasi wanawake wazawa ambapo kwa mwaka wa fedha 2024/25 jumla ya miradi minne
(4) yenye urefu wa kilometa 20 yenye thamani ya Shilingi milioni 53,627.123 imetengwa kwa Makandarasi wanawake na kwa sasa iko katika hatua za mwisho za ununuzi.
e.Kukamilisha ujenzi na ukarabati wa barabara unaoendelea kwa kiwango cha lami
- 19.Mheshimiwa Spika, Serikali imepata mafanikio makubwa katika kuboresha miundombinu ya barabara na madaraja kwa kuzingatia maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM. Katika kipindi hicho, barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 1,365.87 zimejengwa na kukamilika kwa kiwango cha lami. Barabara hizo ni pamoja na:
- i.Kasulu - Kabingo (km 184);
- ii.Mbinga – Mbamba Bay (km 66);
- iii.Mpemba – Isongole (km 50.3);
- iv.Lusitu - Mawengi (km 50);
- v.Njombe – Moronga Section (km 53.9);
- vi.Moronga – Makete Section (km 53.5);
- vii.Rudewa – Kilosa (km 24);
- viii.Morocco – Mwenge (km 4.3);
- ix.Makutano – Natta (Sanzate) Section (km 50);
- x.Loliondo – Mto wa Mbu (sehemu ya Waso – Sale Jct (km 50);
- xi.Chunya – Makongolosi (km 39);
- xii.Tabora (Usesula) – Koga – Mpanda; Sehemu ya Kwanza: Usesula – Komanga (km 115); Sehemu ya Pili: Komanga- Kasinde (km120) na Sehemu ya Tatu: Kasinde – Mpanda (km 118); na
- xiii.Nyahua-Chaya (km 85.4).
f.Kuanza ujenzi mpya na ukarabati wa barabara kwa kiwango cha lami
- 20.Mheshimiwa Spika, vilevile, barabara mbalimbali zenye urefu wa kilometa 3,140.67 zinaendelea kujengwa kwa kiwango cha lami nchi nzima na zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Maelezo ya kina kuhusu hatua ya utekelezaji wa miradi hiyo imeoneshwa kuanzia Aya 48 hadi 142.
g.Miradi ya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina
- 21.Mheshimiwa Spika, Serikali imekamilisha Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa kilometa 3,848.13 kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara kuu na za mikoa. Aidha, usanifu wa madaraja mapya manne (4) ambayo ni Godegode (Dodoma), Mkundi (Morogoro), Malagarasi Chini (Kigoma) na Mirumba (Katavi) pamoja na Upembuzi
Yakinifu wa kilometa 365 kwa ajili ya ukarabati wa barabara kuu na za mikoa kwa kiwango cha lami umekamilika. Vilevile, Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa jumla ya kilometa 3,694.64 upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
h.Ujenzi wa Madaraja
- 22.Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho, jumla ya madaraja makubwa nane (8) yamekamilika. Madaraja hayo ni; Kitengule (Kagera), Wami (Pwani), Msingi (Singida), Tanzanite (Dar es Salaam), Kiyegeya (Morogoro), Gerezani (Dar es Salaam), Mpwapwa (Dodoma) na Ruhuhu (Ruvuma). Aidha, ujenzi wa daraja la Kigongo – Busisi (JP. Magufuli) unatarajiwa kukamilika mapema mwezi Mei, 2025.
- 23.Mheshimiwa Spika, Vilevile, madaraja mengine makubwa 17 yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi, ambayo ni; Mirumba, Pangani, Mbangala, Simiyu, Mbambe, Doma, Nzali, Chakwale, Nguyami, Suguta, Sukuma, Jangwani, Mwanjiri, Mkili, Kalebe, Kavuu, na Mitomoni. Aidha, Madaraja makubwa saba
(7) ya Mpiji Chini, Kibakwe, Kerema Maziwa, Sanza, Munguli na Godegode yako kwenye hatua mbalimbali za maandalizi ya kazi za ujenzi.
- 24.Mheshimiwa Spika, kupitia hadhira hii, naomba kutoa pongezi na shukrani kubwa kwa Mheshimiwa Rais, kwa kutoa fedha zilizowezesha kukamilika kwa mradi wa kimkakati wa ujenzi wa Daraja la Kigongo - Busisi. Wakati Mheshimiwa Rais anaingia madarakani utekelezaji wake ulikuwa umefikia asilimia 25 na ndani ya miaka minne amefanikisha Mkandarasi kulipwa kwa wakati jumla
ya Shilingi Bilioni 539.28 na kukamilisha ujenzi wa daraja hili la kielelezo. Kukamilika kwa daraja hili kutakuwa faraja kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa ambao wamekuwa wakitumia muda wa takriban masaa mawili (2) kuvuka kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine. Baada ya daraja kukamilika muda wa kuvuka unatarajiwa kupungua kutoka masaa mawili (2) hadi wastani wa dakika tatu (3).
i.Kupunguza msongamano katika Jiji la Dar es Salaam
- 25.Mheshimiwa Spika, jumla ya kilometa 52.5 za barabara za kupunguza msongamano wa magari Jijini Dar es Salaam zimejengwa kwa kiwango cha lami. Barabara zilizokamilika ni pamoja na:
- i.Barabara ya Kimara – Kibaha (19.2)
- ii.Barabara ya Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya II kutoka Maktaba – Mbagala (km 19.3)
- iii.Barabara ya Ardhi – Makongo (km 4)
- iv.Barabara ya Wazo Hill – Madale (km 9).
- v.Daraja la Tanzanite (km 1.03).
- vi.Madaraja ya juu ya Chang’ombe na Uhasibu.
Vilevile, miradi inayoendelea kutekelezwa ni pamoja na:
- i.Ujenzi wa Barabara za Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya III kutoka Maktaba – JNIA - Gongolamboto (km 23.3);
- ii.Ujenzi wa Barabara za Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya IV kutoka Maktaba – Morocco – Mwenge - Tegetana Mwenge -
Ubungo (km 30.1); na
- iii.Maandalizi ya kuanza ujenzi wa Barabara za Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya V kutoka
Ubungo – Bandarini, Makutano ya Tabata – Tabata Segerea na Tabata – Kigogo (km 27.6).
Aidha, Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina kwa ajili ya ujenzi wa barabara za juu katika makutano ya Buguruni (Mandela/Uhuru), Magomeni, Fire, Ally Hassan Mwinyi/UN, Ally Hassan Mwinyi/ Kinondoni, Mwenge na Morocco umekamilika. Wizara ya Ujenzi inaendelea na majadiliano na JICA ili kuweza kufadhili ujenzi wa flyovers mbili katika makutano ya barabara ya Ally Hassan Mwinyi na Sam Nujoma (Mwenge) pamoja na makutano na barabara ya Kawawa (Morocco).
j.Kupunguza msongamano katika Majiji mengine
- 26. Mheshimiwa Spika, katika Jiji la Dodoma, jumla ya kilometa 70 kati ya 112.3 za barabara ya Mzunguko wa Nje zimekamilika. Vilevile Serikali inaendelea na taratibu za ununuzi ya Mkandarasi wa ujenzi wa barabara ya Dodoma – Morogoro (Kimbinyiko R/ About – Chamwino Jct km 32). Aidha, kwa barabara ya Dodoma – Iringa (Bahi Rd R/About - Mkonze km 8.5) na Dodoma – Arusha (Bahi Rd R/About – Msalato Airport Jct km 10.7) upembuzi wa awali unaendelea chini ya mradi wa Dodoma Intergrated and Sustainable Transport (DIST) unaopokea mkopo kutoka Benki ya Dunia.
Kukamilika kwa miradi hii kutachochea shughuli za kiuchumi na kijamii kwa watumiaji wa barabara hizo. Natoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kutoa fedha za ujenzi wa barabara hizi muhimu.
- 27.Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Jiji la Mbeya, upanuzi wa sehemu ya Uyole – Ifisi – Songwe Airport (km 36) unaendelea. Aidha, katika mji wa Iringa, ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Mchepuo wa Iringa (km 7.3) unaendelea.
k.Udhibiti uzito wa magari na masuala ya usalama barabarani
- 28.Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TANROADS imeendelea kutekeleza ilani ya CCM kwa kujenga na kuboresha mizani ya kupima magari ili kulinda barabara zisiharibike mapema na kuimarisha udhibiti wa uzito wa magari na kupunguza muda wa upimaji kwa kufanya yafuatayo:
- i.Kufunga mizani ya kisasa (Electronic load cells) ambayo hutoa taarifa ya mwenendo mzima wa hali ya mizani wakati gari linapimwa ili kupata vipimo sahihi katika mizani. Hadi sasa, Load Cell za kidigitali zimefungwa katika mizani kumi (10) ambayo ni Mpemba, Njuki, Mikese North, Mikese South, Mikumi North, Nala, Makuyuni, Mutukula, Mingoyo na Himo II.
- ii.Kufunga mfumo wa kielektroniki ambao unawezesha magari kupimwa kwenye mizani bila kuwa na operator (human intervention). Hadi sasa, mizani 20 ya kupima magari yakiwa kwenye mwendo (Weigh-in-Motion) imefungwa katika vituo vya mizani vya Vigwaza, Mikese, Mikumi, Wenda, Mpemba, Nala, Njuki, Kimokouwa, Dakawa na Rubana.
l.Miradi ya Nyumba na Majengo ya Serikali
- 29.Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanzia mwaka 2020 hadi 2025, Serikali kupitia Wakala wa Majengo (TBA) imekamilisha ujenzi na usimamizi wa jumla ya majengo ya ofisi za Serikali 321 zikiwemo 19 zilizojengwa katika mji wa Serikali Mtumba - Dodoma pamoja na nyumba 2,685 za Watumishi wa Umma katika mikoa mbalimbali. Aidha, Serikali imekamilisha mradi wa kimkakati wa ujenzi wa Ikulu ya Chamwino. Vilevile, ukarabati wa Karakana sita (6) za kutengeneza samani katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Dodoma, Tabora, Mwanza na Mbeya uko katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
- 30.Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanzia mwaka 2020 hadi 2025 Serikali kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), imekamilisha miradi ifuatayo iliyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM mwaka 2020: Kusimika Mfumo wa kielektroniki wa kukusanya mapato katika kituo cha Magogoni - Kigamboni pamoja na maboresho ya Mfumo wa tiketi za kielektroniki katika kituo cha Kigongo – Busisi. Aidha, Serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi ya ununuzi wa vivuko vipya ambavyo utekelezaji wake umefikia hatua zifuatazo; Bwiro-Bukondo (asilimia 92), Kisorya-Rugezi (asilimia 90), Ijinga - Kahangala (asilimia 90), Nyakaliro -Kome (asilimia 90) na Mafia - Nyamisati (asilimia 35).
- 31.Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kujenga na kuboresha miundombinu ya viwanja vya ndege nchini. Viwanja vya ndege vilivyokamilika ni: Ujenzi na ukarabati wa kiwanja cha ndege cha Songwe, Mtwara, Songea, Iringa Awamu ya I na kiwanja cha ndege cha Geita.
- 32.Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa miradi mingine ya viwanja vya ndege ni kama ifuatavyo: Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Package I (asilimia 87) na Package II (asilimia 53.2); Kiwanja cha Ndege cha Kigoma (asilimia 20); Kiwanja cha Ndege cha Tabora (asilimia 93), Kiwanja cha Ndege cha Sumbawanga (asilimia 60), Kiwanja cha Ndege cha Shinyanga (asilimia 80) na Kiwanja cha Ndege cha Musoma (asilimia 58).
- C.MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA WIZARA NA TAASISI ZAKE KWA MWAKA WA FEDHA 2024/25
33.Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikio yaliyopatikana kutokana na utekelezaji wa Ilaniya CCM, Wizara pia imeendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Mpango Mkakati wa Wizara, Mipango Mingine ya Kitaifa na maelekezo ya Viongozi Wakuu wa Kitaifa. Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2024/25 ni kama ifuatavyo.
C.1: MATUMIZI YA FEDHA
Bajeti ya Matumizi ya Kawaida
- 34.Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2024/25, Wizara ya Ujenzi ilitengewa Shilingi 81,407,438,000.00 ikiwa ni Bajeti ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo, Shilingi 76,588,233,000.00 ilikuwa ni Bajeti ya Mishahara na Shilingi 4,819,205,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo.
- 35.Mheshimiwa Spika, hadi Aprili, 2025 jumla ya Shilingi 63,506,309,562.24 zilipokelewa. Kati ya fedha hizo, Shilingi 61,152,975,329.92 ni kwa ajili ya Mishahara ya Watumishi wa Wizara na Taasisi na Shilingi 2,353,334,232.32 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo ya Wizara na Taasisi zake.
Bajeti ya Miradi ya Maendeleo
- 36.Mheshimiwa Spika, Bajeti kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo iliyotengwa kwa mwaka wa fedha 2024/25 kwa Wizara ya Ujenzi ni Shilingi 1,687,888,714,000.00. Kati ya fedha hizo, Shilingi 1,141,803,989,000.00 ni fedha za ndani na Shilingi 546,084,725,000.00 ni fedha za nje. Kati ya fedha za ndani, Shilingi 599,756,467,800.00 ni fedha zilizotengwa kwa ajili ya bajeti ya Mfuko wa Barabara na Shilingi 542,047,521,200.00 ni fedha kutoka katika Mfuko Mkuu wa Serikali.
- 37.Mheshimiwa Spika, hadi Aprili, 2025 fedha zilizopokelewa ni Shilingi 1,535,092,021,470.55. Kati ya fedha hizi, Shilingi 944,881,583,335.76 ni fedha za ndani na Shilingi 590,210,438,134.79 ni fedha za nje. Kati ya fedha za ndani zilizopokelewa, Shilingi 482,085,328,011.98 ni kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali na Shilingi 462,796,255,323.78 ni za Mfuko wa Barabara.
C.2: UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO
Miradi ya Ujenzi na Ukarabati wa Barabara na Madaraja
- 38.Mheshimiwa Spika, Wizara ya Ujenzi kupitia TANROADS inasimamia mtandao wa barabara wenye urefu wa kilometa 37,435.04. Kati ya hizo kilometa 12,527.44 ni barabara kuu na kilometa 24,907.60 ni barabara za mikoa.
- 39.Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2024/25, miradi ya barabara kuu iliyopangwa kutekelezwa ni ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara zenye urefu wa kilometa 385, ukarabati wa kilometa 35 kwa kiwango cha lami, ujenzi wa madaraja 17, ukarabati wa daraja moja (1), maandalizi ya ujenzi wa madaraja tisa (9) na Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa madaraja mawili (2).
- 40.Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili, 2025, ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara zenye urefu wa kilometa 109.49 umekamilika na ujenzi wa kilometa 275.51 unaendelea.
Kwa upande wa madaraja, ujenzi wa madaraja matano (5) unaendelea na ujenzi wa madaraja matano (5) upo katika hatua za maandalizi. Vilevile, taratibu za ununuzi ya Makandarasi wa ujenzi wa madaraja matano (5) zinaendelea. Aidha, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa madaraja 11 na ukarabati wa daraja 1 katika mikoa mbalimbali nchini.
- 41.Mheshimiwa Spika, miradi ya barabara za mikoa iliyopangwa kutekelezwa ni ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara zenye urefu wa kilometa 98, ukarabati kwa kiwango cha changarawe wa barabara zenye urefu wa kilometa 925 pamoja na ujenzi na ukarabati wa madaraja/ makalavati 107.
- 42.Mheshimiwa Spika, hadi Aprili, 2025 jumla ya kilometa 98.13 za barabara za mikoa zilijengwa kwa kiwango cha lami na jumla ya kilometa 192.9 zilikarabatiwa kwa kiwango cha changarawe. Aidha, ujenzi/ukarabati wa madaraja madogo 7 kwa kutumia fedha za Mfuko Mkuu wa Serikali na 9 kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara umekamilika na madaraja 91 yapo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
Miradi ya Matengenezo ya Barabara na Madaraja
- 43.Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2024/25, Wizara kupitia TANROADS ilipanga kufanya matengenezo ya barabara kuu na barabara za Mikoa ambayo yalihusisha matengenezo ya kawaida (routine and recurrent maintenance) kwa kilometa 35,095.63, matengenezo ya muda maalum kilometa 3,206.63, matengenezo ya sehemu korofi kilometa 383.84 pamoja na matengenezo ya madaraja 2,904.
Hadi kufikia Aprili, 2025, kazi zilizofanyika ni matengenezo ya kawaida kilometa 16,533.79, matengenezo ya muda maalum kilometa 1,167.97 matengenezo ya sehemu korofi kilometa 120.72 pamoja na matengenezo ya madaraja 1,358.
- 44.Mheshimiwa Spika, vilevile, Wizara ilipanga kuendelea na udhibiti wa uzito wa magari, kazi za dharura pamoja na mradi wa matengenezo ya barabara kwa mikataba ya muda mrefu.
- 45.Mheshimiwa Spika, hadi Aprili, 2025 jumla ya magari 8,344,978 yalikuwa yamepimwa katika mizani 79 iliyopo nchini ambapo kati ya hayo, magari 22,585 sawa na asilimia 0.27 yalikuwa yamezidisha uzito zaidi ya asilimia 5 ya uzito unaoruhusiwa kisheria. Wasafirishaji waliozidisha uzito walichukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
- 46.Mheshimiwa Spika, miradi saba (7) ya barabara iliyokuwa itekelezwe kwa utaratibu wa EPC
+F sasa inatekelezwa kwa utaratibu wa ‘sanifu na jenga’ (Design and Build). Hadi sasa, addendum za maboresho ya miradi sita (6) zimeshasainiwa. Aidha, mradi mmoja wa Igawa – Songwe – Tunduma sasa utatekelezwa kwa njia wa PPP, ambapo taratibu za kusaini mkataba zinaendelea. Sambamba na hilo, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa ziara yake Mkoani Tanga aliagiza ujenzi wa barabara ambayo hapo awali ilikuwa itekelezwe kwa utaratibu wa EPC+F kutoka Kiberashi hadi Singida sasa utekelezwe kwa utaratibu wa PPP. Tayari TANROADS na TPA wameanza majadiliano kuhusu namna bora ya utekelezaji wa agizo hilo.
- 47.Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa miradi yote ya barabara na madaraja iliyotengewa fedha kwa mwaka 2024/25 hadi kufikia Aprili, 2025 ni kama ifuatavyo:
- 48.Mheshimiwa Spika, taratibu za ununuzi kwa ajili ya kumpata Mkandarasi na Mhandisi Mshauri kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Soni – Bumbuli – Dindira – Korogwe (km 74) sehemu ya Soni – Bumbuli – Funta (km 30) na Kwameta – Kwashemshi (km 10) zinaendelea kufuatia kutangazwa upya kwa zabuni ya ujenzi.
- 49.Mheshimiwa Spika, katika barabara ya Mtwara – Newala – Masasi (km 210), ujenzi kwa kiwango cha lami wa sehemu za Mnivata – Mitesa (km 100) umefikia asilimia 18 na Mitesa – Masasi (km 60) umefikia asilimia 26. Vilevile, taratibu za ununuzi wa kuwapata Makandarasi wa ujenzi wa barabara za Mangamba – Madimba - Msimbati (km 35) na Namichiga – Ruangwa (km 20.6) zinaendelea baada ya kufanya marejeo ya usanifu.
- 50.Mheshimiwa Spika, kwa barabara ya Likuyufusi – Mkenda (km 122.50), Mkataba wa ujenzi wa barabara hii sehemu ya Likuyufusi – Muhukuru (km 60) utasainiwa mwishoni mwa Mei, 2025.
- 51.Mheshimiwa Spika, mkataba wa EPC+F kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Nachingwea – Liwale (130km) umeboreshwa na kuwa Sanifu Jenga (Design and Build). Ujenzi wa barabara hii utafanyika kwa awamu kwa kuanzia sehemu ya Liwale – Kihangara (km 55), ambapo mkandarasi anaendelea na maandalizi ya kuanza ujenzi kwa kutumia fedha za ndani.
- 52.Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabara ya Ubena Zomozi – Ngerengere (km 11), umeanza na unaendelea.
- 53.Mheshimiwa Spika, ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya TAMCO – Vikawe – Mapinga (km 24) unafanyika kwa awamu ambapo ujenzi wa kilometa 4.7 umekamilika na ujenzi wa kilometa 3.6 umefikia asilimia 60. Aidha, ujenzi wa sehemu ya Pangani – Mapinga (km 13.59) umefikia asilimia 11. Vilevile, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya Makofia – Mlandizi (km 36.7).
- 54.Mheshimiwa Spika, kuhusu barabara ya Musoma – Makojo – Busekela (km 92), taratibu za ununuzi ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa sehemu ya Musoma – Kusenyi (km 40) kwa kiwango cha lami zipo hatua za mwisho kwa ajili ya kusaini mkataba wa ujenzi.
- 55.Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabara ya Kongwa Jct – Mpwapwa – Gulwe – Kibakwe (km 98) unafanyika kwa awamu. Hadi Aprili, 2025, ujenzi wa sehemu ya Mpwapwa – Idilo (km 3) ulikuwa umekamilika. Aidha, ujenzi wa sehemu ya Kongwa Jct – Ngambi – Mpwapwa (km 32) upo katika hatua za awali za kuanza ujenzi. Vilevile, Mkataba wa ujenzi wa sehemu ya Mpwapwa – Gulwe – Kibakwe (km 46.9) upo tayari kusainiwa.
- 56.Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabara ya Muhutwe – Kamachumu – Muleba (km 154) kwa kiwango cha lami unafanyika kwa awamu ambapo kilometa 43.55 zimekamilika; ujenzi wa sehemu ya Ilambika - Kalela unaendelea na umefikia asilimia 10.
- 57.Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabara ya Iringa –Ruaha National Park (km 104) upo katika hatua za awali. Aidha, ujenzi wa barabara ya Iringa
(Ipogolo) – Kilolo (km 33.2) kwa kiwango cha lami umefikia asilimia 50.
- 58.Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabara ya Muheza – Amani (km 36) kwa kiwango cha lami unafanyika kwa awamu ambapo ujenzi wa sehemu ya Kwemhosi – Bombani (km 4) umefikia asilimia 98.
- 59.Mheshimiwa Spika, katika mradi wa ukarabati kwa kiwango cha lami wa barabara ya Mtwara – Mingoyo – Masasi (km 200.51), mikataba ya ujenzi wa sehemu za Mtwara – Mingoyo (km 82.27) na Mingoyo – Nanganga – Masasi (km 118.24) imesainiwa. Hivi sasa, Makandarasi wanaendelea na maandalizi ya kuanza kazi za ukarabati.
- 60.Mheshimiwa Spika, kuhusu barabara ya Kibaoni – Majimoto – Muze – Kilyamatundu (km 189), hadi kufikia Aprili, 2025, ujenzi wa sehemu ya Ntendo – Kizungu (km 25) kwa kiwango cha lami unaendelea na umefikia asilimia 50. Aidha, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa sehemu ya Kizungu – Muze (km 12) na barabara ya Kibaoni – Majimoto – Inyonga (km 152).
- 61.Mheshimiwa Spika, hadi mwezi Aprili ujenzi wa Daraja la J.P. Magufuli (Kigongo – Busisi) na barabara Unganishi ulikuwa umefikia asilimia 99. Aidha, ujenzi wa barabara ya Kagera Sugar Jct – Kakunyu; Sehemu ya Kagera Sugar Jct – Kitengule Jct (km 25) unaendelea. Mkataba wa ujenzi wa daraja la Mzinga (Dar es Salaam) ikihusisha upanuzi wa barabara ya Mbagala Rangi Tatu - Kongowe (km 3.8) umesainiwa tarehe 19 Machi, 2025. Aidha, Serikali inaendelea kutafuta fedha za ujenzi wa daraja
la Ugalla (Katavi).
- 62.Mheshimiwa Spika, kazi ya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa barabara ya Morogoro – Dodoma pamoja na Daraja la Mkundi imekamilika. Maandalizi ya kutangaza zabuni za ujenzi wa barabara ya SUA Main Gate – Mzinga Factory Gate (km 11) kwa kiwango cha lami yanaendelea.
- 63.Mheshimiwa Spika, katika barabara ya Njombe – Makete – Isyonje (km 157.4), ujenzi wa sehemu ya Isyonje – Makete (km 50) sehemu ya Kitulo – Iniho (km 36.3) unaendelea na umefikia asilimia 15. Vilevile, ujenzi wa sehemu ya Njombe – Njombe Referral Hospital (km 3) unaendelea kwa awamu ambapo mita 900 zimekamilika.
- 64.Mheshimiwa Spika, kuhusu barabara ya Omugakorongo – Kigarama – Murongo (km 105), taratibu za ununuzi wa Mkandarasi wa ujenzi wa sehemu ya Businde – Murongo (km 53.4) zipo katika hatua za mwisho kwa ajili ya kusaini Mkataba.
- 65.Mheshimiwa Spika, kwa barabara ya Nanganga – Ruangwa – Nachingwea (km 145), ujenzi kwa kiwango cha lami wa sehemu ya Nanganga – Ruangwa (km 53.2) umefikia asilimia 83 na kwa sehemu ya Ruangwa – Nachingwea (km 55.7) umefikia asilimia 3. Kwa sehemu ya Nangurukuru – Liwale (km 210), taratibu za ununuzi ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi kwa kiwango cha lami sehemu ya Choya – Liwale (km 72) zipo katika hatua za mwisho kwa ajili ya kusaini Mkataba. Vilevile, katika barabara ya Masasi – Nachingwea (km 45), mkataba
wa EPC+F umeboreshwa na kuwa Sanifu Jenga (Design and Build) na kuanza ujenzi wa barabara hii kwa awamu kwa kuanzia sehemu ya Liwale – Kihangara (km 55) ambapo mkandarasi anaendelea na maandalizi ya kuanza ujenzi kwa kutumia fedha za ndani.
- 66.Mheshimiwa Spika, katika barabara ya Katumbasongwe – Kasumulu – Ngana – Ileje (km 90.1), ujenzi wa sehemu ya Isongole II – Ndembo (km 46) na Ndembo Spur Road (km 6) upo katika hatua za awali. Aidha, majadiliano na Mkandarasi kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami kwa barabara ya Mlowo – Kamsamba (km 10) yanaendelea. Vilevile, taratibu za ununuzi ya Mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Ukaguzi (Iboya OSIS) zinaendelea kwa kuzingatia marejeo ya usanifu .
- 67.Mheshimiwa Spika, taratibu za kusaini mkataba kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa sehemu ya Ruanda – Iyula – Nyimbili (km 21) zinaendelea. Barabara hii itajengwa na Makandarasi Wanawake ikiwa ni mkakati wa kuwajengea uwezo. Aidha, kwa sehemu ya Chang’ombe – Mkwajuni – Makongolosi (km 61), majadiliano na Mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa sehemu ya kilometa 5 kuanzia Mkwajuni – Makongolosi yanaendelea.
- 68.Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Uyogo – Nyamilangano – Nyandekwa – Kahama (km 54).
- 69.Mheshimiwa Spika, kuhusu ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Sengerema – Nyehunge (km 54), ununuzi ya kumpata Mkandarasi mpya unaendelea baada ya kusitisha mkataba na Mkandarasi wa awali. Aidha, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara ya Kamanga – Katunguru – Sengerema (km 35) kwa kiwango cha lami.
- 70.Mheshimiwa Spika, kwa upande wa barabara ya Omurushaka – Nkwenda – Murongo (km 125), ujenzi wa sehemu ya Kyerwa – Chonyonyo (km 50) unaendelea. Aidha, taratibu za ununuzi kwa ajili ya kumpata Mhandisi Mshauri wa kufanya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina kwa sehemu iliyobaki ya kilometa 75 zinaendelea.
- 71.Mheshimiwa Spika, katika mradi wa Upanuzi wa barabara Kuu zinazoingia katikati ya Jiji la Dodoma (km 51.2), taratibu za ununuzi ya Mkandarasi wa ujenzi wa barabara ya Dodoma – Morogoro (Kimbinyiko R/ About – Chamwino Jct km 32) zinaendelea. Aidha, kwa barabara ya Dodoma – Iringa (Bahi Rd R/About - Mkonze km 8.5) na Dodoma – Arusha (Bahi Rd R/About – Msalato Airport Jct km 10.7) upembuzi wa awali unaendelea chini ya mradi wa Dodoma Intergrated and Sustainable Transport (DIST).
- 72.Mheshimiwa Spika, ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Ntyuka Jct – Mvumi Hospital – Kikombo Jct (km 76.07), sehemu ya Ntyuka Jct – Ntyuka (km 8) na Kikombo Jct – Mapinduzi (km 16.4) umefikia asilimia 53. Aidha, ujenzi wa barabara ya Ntyuka – Mvumi Hospital - Kikombo (km 53) upo katika hatua za awali. Vilevile, Usanifu wa Kina wa
barabara za Ihumwa – Hombolo - Mayamaya (km 60) unaendelea. Kwa Barabara ya kuingia Hospitali ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) Msalato (km 5.5) taratibu za ununuzi ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi zinaendelea.
- 73.Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabara ya Tarime – Mugumu (km 87.14) kwa kiwango cha lami, sehemu ya Mogabiri – Nyamongo (km 25) unaendelea na umefikia asilimia 54. Aidha, Mkandarasi wa ujenzi wa sehemu za Tarime – Mogabiri (km 9.3), Nyamongo – Mugumu (km 48.15) na Barabara unganishi ya Mugumu Roundabout (km 3.6) ameshakabidhiwa eneo la mradi na hivi sasa anaendelea na maandalizi ya kuanza ujenzi. Kwa upande wa barabara ya Mika – Utegi – Shirati – Kirongwe (km 56.8), zabuni za ujenzi sehemu ya Utegi – Shirati (km 27) zimetangazwa na tathmini ya kumpata Mkandarasi kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami zinaendelea.
- 74.Mheshimiwa Spika, Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina kwa ajili ya ukarabati kwa kiwango cha lami wa barabara ya Shelui – Nzega (km 123) unaendelea. Aidha, taratibu za ununuzi kumpata Mkandarasi na Mhandisi Mshauri kwa ajili ya ujenzi wa sehemu ya Shelui – Sekenke – Tulya – Tyegelo (km 62); sehemu ya Shelui – Sekenke – Ntwike (km 20) zinaendelea.
- 75.Mheshimiwa Spika, katika barabara ya Nzega – Kagongwa (km 65), kwa sehemu ya Kagongwa – Sojo (km 18) Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina umekamilika. Aidha, ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Isabdula (Magu) – Bukwimba Station – Ngudu–Ng’hungumalwa(km50);sehemuya
Isabdula – Bukwimba Station (km 10) umefikia asilimia 5. Vilevile, ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Mwanangwa – Misasi – Salawe – Kahama (km 136); sehemu ya km 3 kutoka Mwanangwa unaendelea na umefikia asilimia 40.
- 76.Mheshimiwa Spika, katika barabara ya Mafinga – Mgololo (km 81), mkataba wa EPC+F umeboreshwa na kuwa Sanifu Jenga (Design and Build). Mkandarasi anaendelea na maandalizi ya kuanza ujenzi kwa kutumia fedha za ndani. Aidha, Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa barabara ya Nyololo – Mtwango (km 40.4) umekamilika. Serikali inaendelea kutafuta fedha ili kuijenga barabara hii kwa kiwango cha lami.
.
- 77.Mheshimiwa Spika, ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Singida – Sepuka – Ndago (km 77.4) unaendelea.
- 78.Mheshimiwa Spika, kuhusu mradi wa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Kitai – Lituhi (km 90.0) pamoja na daraja la Mnywamaji, ujenzi wa barabara hii sehemu ya Amanimakoro – Ruanda (km 35) unaendelea na umefikia asilimia 37. Aidha, Mkandarasi wa sehemu ya Ruanda – Ndumbi Port (km 50) ameshakabidhiwa eneo la mradi na hivi sasa anaendelea na maandalizi ya kuanza ujenzi.
- 79.Mheshimiwa Spika, kuhusu barabara za Kuelekea Katika Vituo vya Reli ya Kisasa ya SGR (km 87.6), ujenzi wa barabara ya Kizota – Zuzu SGR Station (km 14) unaendelea na umefikia asilimia 77. Vilevile, ujenzi wa barabara za Morogoro – Kihonda SGR Station (km 10) na Rudewa – Kilosa SGR Station
(km 3) upo katika hatua za awali. Aidha, taratibu za ununuzi katika barabara za Gulwe – Gulwe SGR Station (km 2), Igandu – Igandu SGR Station (km 27), Ihumwa – Ihumwa Marshalling Yard (km 5.50), Bahi – Bahi SGR Station (km 4) na barabara za ndani za kituo cha SGR cha Dodoma (Access Roads to Dodoma SGR Station) zinaendelea. Katika barabara ya Mlandizi – Ruvu SGR Station (km 22) Mkataba wa ujenzi upo tayari kusainiwa.
- 80.Mheshimiwa Spika, katika barabara ya Tanga – Pangani – Makurunge (km 174.5), ujenzi wa sehemu ya Tanga – Pangani (km 50) unaendelea na umefikia asilimia 77. Ujenzi wa sehemu ya Pangani – Mkange (km 124.5) sehemu ya Tungamaa – Mkange (km 95.2) umefikia asilimia 47 na ujenzi wa daraja la Pangani umefikia asilimia 55. Aidha, kazi ya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa barabara ya Mkata – Kwa Msisi (km 36) inaendelea.
- 81.Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabara ya Kisarawe – Maneromango – Mloka (km 150.46) sehemu ya Kisarawe - Maneromango (km 54) kwa kiwango cha lami unafanyika kwa awamu. Hadi Aprili, 2025 kilometa 24.25, ujenzi kwa kiwango cha lami, sehemu ya Kisarawe – Sungwi – Kisanga ( km 27.65) umekamilika. Aidha, kwa sehemu ya Sungwi – Masaki (km 2.1) ujenzi umefikia asilimia 25. Vilevile, mkataba wa ujenzi kwa sehemu ya Masaki – Maneromango (km 34.5) unatarajiwa kusainiwa mwishoni mwa mwezi Mei, 2025.
- 82.Mheshimiwa Spika, kuhusu barabara ya Geita – Bulyanhulu – Kahama (km 120), hadi kufikia Aprili, 2025 ujenzi sehemu ya Kahama - Bulyanhulu Jct –
Kakola (km 73) umefikia asilimia 7. Aidha, mkataba kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Geita – Bukoli (km 57.4) na barabara ya kuingia mji wa Bukoli (km 3.8) unatarajiwa kusainiwa mwishoni mwa mwezi Mei, 2025. Vilevile, taratibu za manunuzi kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami kwa sehemu za Nyikonga – Kashelo (km 10.5), Kashelo – Ilolangulu (km 15) na Ushirombo – Kilimahewa – Nanda (km 15.7) zinaendelea.
- 83.Mheshimiwa Spika, katika barabara ya Nyamirembe Port – Katoke (km 50); kwa sehemu ya Nyamirembe Port – Nyamirembe Jct (km 1.7) ujenzi kwa kiwango cha lami unaendelea na umefikia asilimia 25. Kwa sehemu ya SIDO – Chato Zonal Hospital (km 5.3) ujenzi umefikia asilimia 12.
- 84.Mheshimiwa Spika, katika Barabara ya Geita – Nzera - Nkome (km 54); sehemu ya Sungusila - Nzera – Nkome (km 20.36) ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami upo katika hatua za awali.
- 85.Mheshimiwa Spika, katika mradi wa Arusha – Moshi – Himo – Holili (km 199.51), ujenzi wa barabara ya Mianzini – Ngaramtoni (km 18) umefikia asilimia 48. Aidha, kazi ya Usanifu wa Kina wa barabara ya Tengeru – USA River (km 9.3), Daraja Jipya la Kikafu (m 560) pamoja na Barabara Unganishi (km 4.06) na Barabara za Moshi Mjini (km 8.4) inaendelea.
- 86.Mheshimiwa Spika, katika mradi wa ujenzi wa barabara za Kuelekea Kwenye Mradi wa Kufua Umeme Katika Maporomoko ya Mto Rufiji, ujenzi wa barabara ya Bigwa – Matombo – Mvuha (km 78) kwa
kiwango cha lami upo katika hatua za awali. Katika barabara ya Ubena Zomozi – Ngerengere (km 11), ujenzi kwa kiwango cha lami umeanza.
- 87.Mheshimiwa Spika, Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa barabara za Ubena Zomozi – Mvuha – Kisaki – Mtemele Jct (km 178); sehemu ya Ngerengere – Mvuha – Kisaki – Mtemele Jct (km 166.4) kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami unaendelea. Vilevile, taratibu za ununuzi kwa ajili ya kumpata Mhandisi Mshauri wa kufanya kazi ya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina katika barabara ya Chalinze – Utete (km 354.9) zipo katika hatua za mwisho. Aidha, kazi za matengenezo ya barabara za Maneromango – Vikumburu – Mloka (km 100) na Kibiti – Mloka – Mtemele – Rufiji JNHHP (km 203) kwa kiwango cha changarawe zinaendelea.
- 88.Mheshimiwa Spika, kazi za ukarabati (overlay) wa sehemu ya Mlandizi – Chalinze (km 44.24) zinaendelea. Ukarabati kwenye Barabara ya Msoga – Msolwa (km 10.2) (Chalinze Bypass) sehemu ya km
7 unaendelea na umefikia asilimia 80. Aidha, kwa sehemu ya Kibaha – TAMCO (km 4.5) maandalizi ya kutafuta Mkandarasi wa upanuzi wa sehemu hii kwa kiwango cha lami zinaendelea ambapo Mhandisi Mshauri yupo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha usanifu pamoja na nyaraka za zabuni.
- 89.Mheshimiwa Spika, kwa upande wa barabara ya Wazo Hill – Bagamoyo – Msata (km 118.10), ukarabati na upanuzi wa sehemu ya Tegeta/Kibaoni – DAWASA/Basihaya (km 2.9) unatekelezwa kupitia mradi wa ujenzi wa Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Nne (BRT IV). Serikali inaendelea kutafuta fedha za
ukarabatinaupanuziwasehemuya
DAWASA/Basihaya – Bagamoyo (km 47).
- 90.Mheshimiwa Spika, kuhusu barabara za Nyakahura – Kumubuga – Rulenge – Kabanga Nickel (km 141) kwa sehemu za Rulenge – Kabanga Nickel (km 32), Kumubuga – Rulenge – Murusagamba (km 75) na Nyakahura – Kumubuga – Murusagamba (km 34), Serikali inaendelea kutafuta fedha za ujenzi wa barabara hizi kwa kiwango cha lami.
- 91.Mheshimiwa Spika, katika mradi wa Kigoma – Kidahwe – Uvinza – Kaliua – Tabora (km 265), ujenzi wa sehemu ya Uvinza – Malagarasi (km 51.1) umefikia asilimia 77.
- 92.Mheshimiwa Spika, katika barabara ya Ifakara – Kihansi – Mlimba – Madeke – Kibena (km 346.43), Makandarasi wa ujenzi kwa kiwango cha lami wa sehemu za Ifakara – Mbingu (km 62.5) na Mbingu – Chita JKT (km 37.5) wameshakabidhiwa maeneo ya mradi na hivi sasa wanaendelea na maandalizi ya kuanza kazi za ujenzi. Katika Barabara ya Njombe (Kibena) – Lupembe – Madeke (km 126); Sehemu ya Kibena – Kidegembye (km 42) taratibu za ununuzi ya Mkandarasi na Mhandisi Mshauri kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami zipo katika hatua za mwisho. Aidha, Mhandisi Mshauri anaendelea na kazi ya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa sehemu ya Kihansi – Mlimba – Madeke (km 95.26).
- 93.Mheshimiwa Spika, katika barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti River – Lalago – Maswa (km 389), kazi za ujenzi wa sehemu ya Mbulu – Garbabi (km 25) zimefikia asilimia 28. Vilevile, Mkandarasi wa ujenzi kwa kiwango cha lami sehemu
ya Labay – Haydom (km 25) ameshakabidhiwa eneo la mradi na hivi sasa anaendelea na maandalizi ya kuanza kazi za ujenzi. Aidha, katika sehemu ya Nkoma – Lalago (km 65), mkataba wa EPC+F umeboreshwa na kuwa Sanifu Jenga (Design and Build). Mkandarasi anaendelea na maandalizi ya kuanza ujenzi kwa kutumia fedha za ndani. Serikali inaendelea kutafuta fedha za ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Mogitu – Haydom (km 68).
- 94.MheshimiwaSpika,kuhusubarabaraya
Marangu–Tarakea–Rongai–Kamwanga
/Bomang’ombe – Sanya Juu (km 105.16), sehemu ya Kwa Sadala – Masama – Machame Junction (km 16), ujenzi wa daraja la Kikafu Juu (m 25) na barabara unganishi (m 400) upo katika hatua za awali. Kwa upande wa barabara ya Kiboroloni – Kiharara – Tsuduni – Kidia (km 10.8) ujenzi unaendelea kwa awamu ambapo jumla ya km 6 zimekamilika na kilometa 1 ipo katika hatua za ununuzi. Aidha, Mikataba ya ujenzi wa sehemu ya Sanya Juu – Kamwanga (Elerai – Kamwanga (km 39.5) na barabara ya Tarakea – Holili (km 53); sehemu ya Munga – Kitangara Mrere (km 10) inatarajiwa kusainiwa mwishoni mwa mwezi Mei, 2025. Vilevile, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ukarabati wa sehemu ya Bomang’ombe – Sanya Juu (km 25).
- 95.Mheshimiwa Spika, katika barabara ya Tukuyu – Mbambo – Katumba (km 60.6), Makandarasi wa ujenzi wa sehemu za Katumba – Lupaso (km 35.3) na Mbaka – Kibanja (km 20.7) wameshakabidhiwa maeneo ya mradi na hivi sasa wanaendelea na maandalizi ya kuanza kazi za ujenzi. Aidha, Serikali inaendelea kutafuta
fedha kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa sehemu ya Mbambo – Ipinda (km 19.7).
- 96.Mheshimiwa Spika, mradi wa ujenzi wa barabara ya Dodoma – Manyoni (km 127) na Barabara ya Kuingia Manyoni Mjini (km 4.8) umekamilika. Mradi huu pia unahusisha ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Ukaguzi (One Stop Inspection Station – OSIS) cha Muhalala (Manyoni). Mkataba wa awali wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa OSIS umesitishwa kutokana na changamoto za kimkataba ambapo utekelezaji wake ulikuwa umefikia asilimia 50. Ujenzi utaendelea baada ya kufikia makubaliano ya stahiki za pande zote mbili. Rasimu ya makubaliano ya stahiki za pande zote mbili imewasilishwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya upekuzi (vetting).
- 97.Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabara ya Tabora – Mambali – Bukene – Itobo (km 114) unafanyika kwa awamu, ambapo ujenzi wa sehemu ya km 1 kutoka kijiji cha Uduka umekamilika. Taratibu za ununuzi sehemu ya mita 400 zipo katika hatua za mwisho za kusaini mkataba.
- 98.Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa Barabara ya Namanyere – Katongoro – New Kipili Port (km 64.8) kwa kiwango cha lami.
- 99.Mheshimiwa Spika, katika barabara ya Dumila – Kilosa – Mikumi (km 141), Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa sehemu ya Kilosa – Ulaya – Mikumi (km 72) kwa kiwango cha lami.
- 100.Mheshimiwa Spika, katika barabara ya Sumbawanga – Matai – Kasanga Port (km 107), ujenzi wa barabara ya Matai – Kasesya (km 50) sehemu ya Matai – Tatanda (km 25) unaendelea na umefikia asilimia 42 na ujenzi wa sehemu ya Tatanda – Kasesya (km 25) upo katika hatua za awali.
- 101.Mheshimiwa Spika, hadi Aprili, 2025, katika mradi wa Ujenzi wa Madaraja Makubwa, ujenzi wa daraja la Mbambe umefikia asilimia 26, Mbangala asilimia 67, Mirumba asilimia 20, Simiyu asilimia 42, Doma asilimia 7, Nzali asilimia 7, Chakwale asilimia 18, Nguyami asilimia 10, Mitomoni asilimia 7 na Sukuma asilimia 33.1. Aidha, ujenzi wa barabara unganishi katika Daraja la Sibiti (Singida) umefikia asilimia 6.
Vilevile, Makandarasi wa ujenzi wa Madaraja ya Mpiji Chini, Kibakwe, Kerema Maziwa, wanaendelea na maandalizi ya ujenzi. Mikataba ya ujenzi wa madaraja ya Sanza, Godegode ipo katika hatua za mwisho za kusainiwa. Usanifu wa Kina wa madaraja ya Munguli na Malagarasi Chini umekamilika. Vilevile, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ukarabati wa daraja la Kirumi na ujenzi wa daraja la Mtera Dam. Aidha, ujenzi wa daraja la Suguti utatekelezwa kupitia mradi wa TANTIP.
- 102.Mheshimiwa Spika, kuhusu barabara ya Kyaka – Bugene – Kasulo (km 183.10), ujenzi wa sehemu ya Bugene – Kasulo – Kumunazi & Kyaka – Mutukula (km 124) sehemu ya Bugene – Burigi Chato National Park (km 60) unaendelea na umefikia asilimia 41.
- 103.Mheshimiwa Spika, katika mradi wa barabara ya Isaka – Lusahunga (km 242), kazi za ukarabati wa sehemu ya Lusahunga – Rusumo (km 92) zinaendelea na zimefikia asilimia 20. Kwa upande wa ujenzi wa Kituo cha Ukaguzi wa Pamoja (OSIS) cha Nyakanazi, mkataba wa awali umesitishwa kutokana na changamoto za kimkataba. Ujenzi utaendelea baada ya ya kufikia makubaliano ya stahiki za pande zote mbili. Rasimu ya makubaliano ya stahiki za pande zote mbili imewasilishwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya upekuzi (vetting).Aidha, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa sehemu ya Nyakasanza – Kobero (km 58).
- 104.Mheshimiwa Spika, Usanifu wa Kina kwa ajili ya ajili ya ukarabati wa barabara ya Mwanza/Shinyanga Border – Mwanza (km 102) kwa kiwango cha lami umekamilika. Hatua za ununuzi kwa ajili ya kumpata Mkandarasi wa upanuzi wa sehemu ya Mwanza - Usagara - JPM Bridge (km 37) kutoka njia mbili hadi njia nne zinaendelea.
- 105.Mheshimiwa Spika, kazi zilizopangwa kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2024/25 kwa ajili ya miradi ya Barabara za Mikoa ni ukarabati wa jumla ya kilometa 600 kwa kiwango cha changarawe, kujenga kilometa
60 kwa kiwango cha lami na ujenzi wa Madaraja/ Makalavati 70.
Hadi kufikia Aprili, 2025, kilometa 117.50 za barabara za mikoa zilikuwa zimekarabatiwa kwa kiwango cha changarawe na kilometa 70.22 zimejengwa kwa kiwango cha lami. Aidha, ujenzi wa madaraja/makalavati 7 umekamilika na yaliyobaki 63 yako katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
- 106.Mheshimiwa Spika, katika mradi wa barabara za kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam, taratibu za ununuzi ya Mkandarasi kwa ajili ya upanuzi wa Barabara ya Mwai Kibaki (km 9.1) na ujenzi wa barabara za Mji Mwema – Kimbiji – Pembamnazi (km 27); sehemu ya km 10 na Mbezi Victoria – Magoe Mpiji (km 9.55); sehemu ya km 6.55 zinaendelea.
- 107.Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabara ya Goba – Matosa – Temboni (km 6) unaendelea kufanyika kwa awamu ambapo kilometa moja (1) imekamilika na ujenzi wa kilometa 5 unaendelea. Vilevile, upanuzi wa barabara ya Kongowe – Mjimwema – Kivukoni Ferry (km 25.1) unaendelea kwa km 1.4 na umefikia asilimia 80, ujenzi wa barabara za Kipata (m 700), Livingstone (m 350) na Msikitini – Sharif Shamba (km 1) unaendelea na umefikia asilimia 85, Kibamba Shule – Mpiji Magoe (km 9.2) umefikia asilimia 95, Chanika – Mbande (km 3.8) umefikia asilimia 75, Mbezi Msakuzi – Makabe Jct (km 8.36) asilimia 90 na Kimara – Bonyokwa – Kinyerezi (km 6.73) unaendelea na umefikia asilimia 13.
- 108.Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Kolandoto – Lalago – Ng’oboko – Mwanhuzi (km 122) kwa awamu.
- 109.Mheshimiwa Spika, kwa barabara ya Ndundu – Somanga (km 60), ujenzi wa barabara ya Utete – Nyamwage (km 33.7) unaendelea na umefikia asilimia 9. Aidha, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ukarabati wa sehemu za Kongowe –
Malendego(km160.65)naNangurukuru– Mbwemkuru (km 95).
- 110.Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa barabara ya Kasulu – Manyovu pamoja na barabara za kuingia Kasulu Mjini (km 68) unaendelea na umefikia asilimia 84.
- 111.Mheshimiwa Spika, kwa upande wa mradi wa barabara ya Mzunguko katika Jiji la Dodoma (Dodoma City Outer Dual Carriageway Ring Road Lot1 & 2 - km 112.3), ujenzi wa sehemu ya Nala – Veyula – Mtumba – Ihumwa Dry Port (km 52.3) unaendelea na umefikia asilimia 86 na ujenzi wa sehemu ya Ihumwa Dry Port – Matumbulu – Nala (km 60) umefikia asilimia 82.
- 112.Mheshimiwa Spika, kuhusu ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Mzunguko wa Ndani katika Jiji la Dodoma: Bahi R/About – Image R/About – Ntyuka R/About – Makulu R/About (km 6.3), majadiliano na Serikali ya Japan kuhusu ugharamiaji wa ujenzi wa barabara hii yanaendelea. Vilevile, kazi ya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa Dodoma City Middle Ring Road inayoanzia Nanenane – Miyuji – Mnadani Sekondari – Mkonze – Ntyuka – Nanenane (km 47.2) umekamilika. Aidha, kazi ya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa barabara ya Msalato – Mtumba – Chamwino IKULU (km 30) inaendelea.
- 113.Mheshimiwa Spika, kwa upande wa barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupiro – Malinyi – Londo – Lumecha/Songea (km 499), kazi za ujenzi kwa kiwango cha lami sehemu ya Kidatu – Ifakara
(km 66.9) na ujenzi kwa kiwango cha changarawe wa barabara za kuelekea mashamba ya wakulima wa miwa ya Mbigiri (km 50) zimekamilika. Vilevile, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Chalinze – Magindu – Lukenge – Seregete B – Kabwe Jct – Mkulazi (km 77.50).
- 114.Mheshimiwa Spika, katika mradi wa ujenzi wa barabara ya Tabora – Ipole – Koga – Mpanda (km 365.36), ujenzi wa barabara ya Mpanda Airport – Kasimba Jct (km 3) umekamilika.
- 115.Mheshimiwa Spika, kuhusu barabara ya Makutano – Natta – Mugumu/Loliondo – Mto wa Mbu (km 185), hadi Aprili, 2025, kazi za ujenzi wa sehemu ya Sanzate – Natta (km 40) zimefikia asilimia
55. Aidha, mkataba wa ujenzi wa barabara ya Wasso – Loliondo (km 10) unatarajiwa kusainiwa mwishoni wa mwezi Mei, 2025. Taratibu za ununuzi za kuwapata Makandarasi wa barabara za Mto wa Mbu – Selela (km 23) na Ngaresero – Engaruka (km 39) kwa kiwango cha lami zinaendelea. Vilevile, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara ya Natta – Mugumu (km 45).
- 116.Mheshimiwa Spika, katika mradi wa Ibanda – Itungi Port/Kajunjumele – Kiwira Port (km 32), kazi za ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Ukaguzi (OSBP) cha Kasumulu/Songwe (Tanzania/Malawi Border) unaendelea na umefikia asilimia 95. Aidha, ukarabati wa barabara ya Ibanda – Itungi Port (km 26) na Kajunjumele (Iponjola) – Kiwira Port (km 6) umefikia asilimia 2 na taratibu za ununuzi ya Mkandarasi mpya zinaendelea baada ya kusitishwa kwa mkataba wa awali kutokana na utendaji usioridhisha wa Mkandarasi.
- 117.Mheshimiwa Spika,