Mkurugenzi wa Idara ya Uendeshaji na Ujenzi wa Vivuko

Mkurugenzi atafanya kazi zifuatazo;

(i) kuunda programu fupi na ndefu za kazi na kusimamia utekelezaji wa programu hizo.

(ii) Kutengeneza mpango sahihi wa kupata vivuko vipya na kuondoa vivuko vilivyokwisha muda wake wa matumizi na kupendekeza juu ya uanzishwaji wa vituo vipya vya kivuko.

(iii) Kutengeneza programu za kujenga uwezo na kuimarisha uwezo wa kiufundi na kiutendaji juu ya shughuli za usalama wa huduma za vivuko

(iv) Kuhakikisha kuwa huduma zote za kivuko zinatolewa kulingana na viwango na taratibu za usalama.