Sehemu ya Huduma za Ushauri

Sehemu hii itafanya shughuli zifuatazo:

(i) Kuendesha huduma za ushauri wa kiufundi.

(ii) Kumsaidia mkurugenzi wa matengenezo na huduma za kiufundi juu ya kazi za ushauri wa umeme, mitambo, elektroniki, TEHAMA na huduma za ushauri.

(iii) Kusimamia watumishi wote wa sehemu ya huduma ya ushauri wa kiufundi.

(iv) Kutengeneza na kusimamia utekelezaji wa mipango kazi ya ushauri wa muda mfupi na muda mrefu kwa kazi za umeme, mitambo, elektroniki, mawasiliano ya simu na kazi za TEHAMA.

(v) Kuanzisha na kukuza sera, mipango na programu zitakazochochea ubora wa bidhaa za umeme na TEHAMA.

(vi) Kuangalia utekelezaji wa kazi za ushauri wa umeme, mitambo, elektroniki na TEHAMA.

(vii) Kuratibu na kujumuisha ripoti za kazi za ushauri wa umeme, mitambo, elektroniki na TEHAMA na kuwasilisha kwa mkurugenzi wa matengenezo na huduma za kiufundi.