Kazi za Kitengo cha TEHAMA na Takwimu

Kutoa huduma ya kitaalamu juu ya takwimu na matumizi ya TEHAMA kwa Wakala.

Kitengo hiki kitafanya shughuli zifuatazo:

(i) Kusimamia mifumo ya kompyuta na kusanikisha programu.

(ii) Kubuni na kutunza Mitandao ya eneo dogo (LAN) na Mitandao ya eneo kubwa (WAN)

(iii) Kusanikisha, kuweka na kubuni teknolojia mpya za huduma za mawasiliano.

(iv) Kushauri juu ya usalama sahihi wa vifaa na data kwa kuhakikisha kuwa vifaa na mifumo vimehifadhiwa vizuri.

(v) Kutunza na kusanikisha mifumo mipya ya tovuti mara kwa mara.

(vi) Kuratibu maendeleo na kuitunza hifadhi data kuu ya Wakala.

(vii) Kuwezesha muundo wa mifumo mipya, kutengeneza na kubuni mifumo ya programu kulingana na mahitaji ya mtumiaji, kurekebisha na kuendeleza mifumo ya kisasa.

(viii) Kubuni, kukuza na kudumisha hifadhi data kulingana na mahitaji maalum ya mtumiaji.

(ix) Kubuni mifumo mipya na salama ya TEHAMA ya ukusanyaji wa data, uhifadhi na uchambuaji wa data na udhibiti.

(x) Kutoa ushauri juu ya wavuti na usanifu wa mifumo ya kompyuta ili kuweka ulinzi katika mifumo na kuhakikisha usalama wa mifumo na viunganisho vya mitandao na pia kuanzisha na kutunza miundombinu ya mtandao na viwango vinavyohitajika vya utendaji.

(xi) Kuwezesha operesheni ya Serikali Mtandao na Biashara Mtandao kwa Wakala.