Kazi za Kitengo cha Huduma za Sheria

Kutoa huduma za kisheria na ushauri kwa Wakala.

Kitengo hiki kitafanya shughuli zifuatazo:

(i) Kutoa ushauri wa kisheria, maoni na mwongozo kwa Wakala.

(ii) Kushauri Wakala juu ya maswala yanayohusu sheria, kanuni na sera za serikali.

(iii) Kutengeneza rasimu, kuhakiki mikataba yote au nyaraka zozote ambazo Wakala unahusika nazo na kukagua athari za kisheria ambazo zinahitaji kuletwa kwa kujadiliwa na menejimenti.

(iv) Kuandaa, kukagua na kurekebisha mikataba ili kusaidia shughuli mbali mbali za biashara za Wakala.

(v) Kuwa msimamizi wa muhuri wa Wakala na hati za mali/ viwanja vya Wakala.

(vi) Kufuatilia majukumu ya kisheria na kushauri menejimenti kuhusu usimamizi ipaswavyo.

(vii) Kuwakilisha na kulinda dhamira ya Wakala katika korti/ mahakama na taasisi za serikali.

(viii) Kuongoza Sekretarieti ya Mikutano ya Bodi ya Ushauri ya Wakala.