Ujumbe wa Mtendaji Mkuu
Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) ni Wakala wa Serikali ulioanzishwa mwaka 2005 kwa ajili ya kutoa huduma za kihandisi katika fani za Umeme, Mitambo na Elektroniki, Ushauri wa Kiufundi na Huduma za Ushauri wa kitaalamu kwenye masuala ya Umeme na Elektroniki, Uendeshaji wa uhakika na usalama wa Vivuko na Ukodishaji wa mitambo ili kusaidia kukuza uchumi wa Tanzania.
Tunasimamia jumla ya vivuko 33 na boti 7 katika vivuko 22 kote nchini ambavyo kwa wastani huhudumia watu milioni 26.8, magari milioni 1.7 na tani 499 za mizigo kila mwaka. Pia tunasimamia na kuendesha karakana 30 kote nchini ambapo tunatengeneza na kuhudumia magari takriban 29,263 kwa mwaka.
Katika uendeshaji wa huduma zetu tunaongozwa na nguzo tatu muhimu;
Ufanisi, Ubunifu na Kuridhika kwa mteja. Tunafurahia kutimiza ahadi hizi kwa kutambua unyeti wa majukumu tuliyokabidhiwa kwa utendaji mzuri wa Serikali na wa watu tunaowahudumia, tunajipa changamoto ya kufanya maboresho ya mara kwa mara katika utoaji wetu wa huduma hizi na tunakutia moyo wewe mteja wetu na umma kwa ujumla, ili kutusaidia kuboresha kwa kutoa maoni kuhusu utoaji wa huduma zetu na maeneo tunayopaswa kuboresha.
Kwa niaba ya menejimenti na wafanyakazi wa Wakala, nawashukuru wote kwa kuendelea kutuunga mkono.
Lazaro N. Kilahala
Mtendaji Mkuu
Huduma bora kwa Fursa za Maendeleo