HOTUBA YA MAKADIRIO YA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2022/2023
Imewekwa Monday 23rd May , 2022
NA UCHUKUZI, MHESHIMIWA
PROF. MAKAME MNYAA MBARAWA(MB), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI
YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
A. UTANGULIZI
1.Mheshimiwa Spika, ninaomba kutoa hoja kwamba, baada ya kupokea taarifa iliyowasilishwa hapa Bungeni na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu iliyochambua utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ya mwaka wa fedha 2021/22, Bunge lako Tukufu likubali kupokea, kujadili na kupitisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2022/23.
2.Mheshimiwa Spika,nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema kwa kutupa kibali cha kukutana leo tukiwa wazima wa afya njema. Aidha, kwa unyenyekevu mkubwa ninamuomba Mwenyezi Mungu atuongoze katika kujadili wasilisho hili la Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi pamoja na bajeti nzima ya Serikali ili kuendelea kuchangia katika maendeleo ya wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
3.Mheshimiwa Spika,naomba kutumia fursa hii kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi uliotukuka ambao ameuonesha tangu alipochukua kijiti cha kuongoza Taifa hili kufuatia kifo cha Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichotokea tarehe 17 Machi, 2021. Uongozi wa Rais wa Awamu ya Sita umedhihirika kuwa wenye umakini wa hali ya juu, utendaji uliotukuka, maono yenye manufaa makubwa kwa Taifa, ujasiri, maarifa na uwajibikaji. Ninamuomba Mwenyezi Mungu amjalie Rais wetu afya njema ili aweze kutekeleza majukumu yake.
4.Mheshimiwa Spika, napenda kumpongeza Makamu wa Rais Mheshimiwa Dkt. Philip Isdory Mpango kwa jinsi anavyoendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ya kuwaletea watanzania maendeleo katika nyanja mbalimbali. Ni wazi kuwa Mheshimiwa Makamu wa Rais ametekeleza majukumu yake kwa umahiri mkubwa na hivyo kuchangia katika maendeleo ya Taifa.
5.Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kiongozi wa shughuli za Serikali hapa Bungeni, kwa uongozi wake mahiri na makini. Sote ni mashuhuda wa kazi iliyotukuka anayoifanya katika utekelezaji wa majukumu yake ndani na nje ya Bunge.
6.Mheshimiwa Spika, kwa heshima kubwa nitoe shukrani zangu za dhati kwa Mheshimiwa Rais kwa imani kubwa aliyokuwa nayo juu yangu kwa kuniteua kuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi tarehe 12 Septemba, 2021. Hii ni mara ya pili ninahudumu katika Wizara hii na ninaahidi kwake na kwa Taifa kwa ujumla kwamba nitaitumikia nafasi hii kwa uadilifu na kwa uwezo wangu wote. Nikiwa kama msaidizi wake katika kusimamia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, natumia fursa hii kumhakikishia kwamba mimi pamoja na wenzangu tutafanya kila linalowezekana kuhakikisha kwamba kazi ya kulijenga Taifa hili inaendelea ili kufikia malengo tuliyojiwekea kupitia miongozo mbalimbali ikiwemo miongozo kupitia Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020.
7.Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kukupongeza wewe binafsi kwa kuchaguliwa kwa kishindo kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu kuwa Naibu Spika. Hakika mnatosha na tuna imani kubwa kwamba chini ya uongozi wenu Bunge hili litatekeleza majukumu yake kwa uadilifu, umahiri na weledi mkubwa. Aidha, niwapongeze Wenyeviti wa Kamati za Bunge kwa namna wanavyolisimamia na kuliongoza Bunge letu Tukufu ili litimize majukumu yake ya kushauri na kuisimamia Serikali.
8.Mheshimiwa Spika, kipekee naomba kuishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu inayoongozwa na Mheshimiwa Seleman Moshi Kakoso, Mbunge wa Mpanda Vijijini, na Makamu Mwenyekiti wa Kamati Mheshimiwa Anne Kilango Malecela, Mbunge wa Same Mashariki pamoja na Wajumbe wote wa Kamati hiyo. Kwa ujumlaKamati imeendelea kutoa ushauri stahiki kwa Wizara na Taasisi zake katika kutekeleza majukumu yake na nikiri kwamba imefanya hivyo kwa ufanisi. Aidha, uchambuzi walioufanya kwenye Taarifa ya Utekelezaji ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2021/22 na Mpango na Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2022/23 umetusaidia kwa kiasi kikubwa kuandaa Bajeti ya Wizara kwa ubora wa hali ya juu. Napenda kuiahidi Kamati hii kwamba Wizara itaendelea kupokea maoni na ushauri wao na kuufanyia kazi kwa kadri inavyowezekana kwa lengo la kuboresha utendaji na kutekeleza kwa ufanisi mipango ya Sekta za Ujenzi na Uchukuzi.
9.Mheshimiwa Spika, sambamba na salamu hizo nichukue fursa hii kutoa mkono wa pole kwa Bunge lako Tukufu kufuatia kifo cha Mbunge mwenzetu Marehemu Elias John Kwandikwa aliyefariki tarehe 02 Agosti, 2021 ambaye hadi umauti unamkuta alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa. Kabla ya hapo, Marehemu aliwahi kuhudumu katika Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kama Naibu Waziri kuanzia mwaka 2016 hadi alipoteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa tarehe 05 Disemba, 2020. Tutaendelea kuienzi michango yake katika ustawi na maendeleo ya Jimbo la Ushetu alilotoka na Taifa kwa ujumla katika nyadhifa za Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa pamoja na Naibu Waziri (Sekta ya Ujenzi). Aidha, ninatoa mkono wa pole kwa Bunge lako Tukufu kufuatia kifo cha Mbunge mwenzetu Marehemu William Ole Nasha ambaye alikuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) na Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro. Marehemu Ole Nasha alifariki tarehe 27 Septemba, 2021. Pia, natoa pole kwa Bunge lako Tukufu kwa kifo cha Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mkoa wa Rukwa, Marehemu Irene Alex Ndyamukama aliyefariki tarehe 24 Aprili, 2022. Tunamuomba Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi, Amina.
10.Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kuwashukuru na kuwapongeza Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), Waziri wa Fedha na Mipango kwa hotuba zao ambazo zimefafanua utendaji wa Serikali kwa mwaka 2021/22 na kutoamwelekeo wa mpango na bajeti kwa mwaka 2022/23. Aidha, nawapongeza Mawaziri wote waliotangulia kwa mawasilisho mazuri ya hotuba za Wizara wanazozisimamia.
11.Mheshimiwa Spika, kabla ya kuwasilishaUtekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2021/22pamoja na Mpango na Bajeti ya Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2022/23, naomba kwa muhtasari niainishe baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika Sekta za Ujenzi na Uchukuzi ndani ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita.
B. MAFANIKIO YA MWAKA MMOJA WA SERIKALI YA AWAMU YA SITA KATIKA SEKTA ZA UJENZI NA UCHUKUZI
12.Mheshimiwa Spika, sote ni mashahidi wa namna Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ilivyopata mafanikio katika sekta mbalimbali. Nitaeleza kwa kifupi mafanikio katika sekta ninazoziongoza ambazo ni Sekta ya Ujenzi na Sekta ya Uchukuzi.
13.Mheshimiwa Spika, majukumu ya msingi ya Sekta ya Ujenzi ni kusimamia utekelezaji wa Sera ya Ujenzi (2003) pamoja na Sera ya Taifa ya Usalama Barabarani (2009); ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara, madaraja na vivuko; ujenzi na uendelezaji wa miundombinu ya viwanja vya ndege; ujenzi na ukarabati wa nyumba na majengo ya Serikali; usimamizi wa masuala ya ufundi na umeme; usimamizi wa shughuli za ukandarasi, uhandisi, ubunifu majengo na ukadiriaji majenzi; usimamizi wa maabara za vifaa vya ujenzi; usimamizi wa masuala ya usalama barabarani na mazingira katika Sekta; uboreshaji, utendaji na uendelezaji wa watumishi wa Sekta pamoja na usimamizi wa majukumu ya taasisi zilizo chini ya Sekta.
14.Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Sekta ya Uchukuzi, majukumu yake ni kusimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uchukuzi (2003); ujenzi na uendelezaji wa miundombinu ya reli na bandari; usafiri na usafirishaji kwa njia ya anga, reli na bandari; utoaji wa leseni za usafirishaji; usalama katika usafirishaji; usimamizi wa huduma za hali ya hewa; kuendeleza rasilimali watu katika Sekta ya Uchukuzi na kusimamia Taasisi na Mashirika ya Umma yaliyo chini ya Sekta ya Uchukuzi.
15.Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kutoa fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo ujenzi wa barabara za juu katika jiji la Dar es Salaam, ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli katika eneo la Kigongo - Busisi mkoani Mwanza, Daraja Jipya la Wami lililopo mkoa wa Pwani, na Daraja Jipya la Selander (Tanzanite) ambalo ujenzi wake umekamilika na limefunguliwatarehe 24 Machi, 2022 na MheshimiwaSamia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Vilevile, mradi wa ujenzi wa nyumba za makazi kwa ajili ya familia 644 za wakazi waMagomeni Kota umekamilika na kufunguliwa rasmi na Mheshimiwa Rais tarehe 23 Machi, 2022. Kukamilika kwa mradi huu kutawawezesha wakazi hao kupata makazi bora na ya kisasa, kutoa fursa za biashara katika maduka na vizimba 186 zilivyomo ndani ya eneo la mradi. Utekelezaji wa mradi huu umezalisha wastani wa ajira 600 kwa siku kwa mafundi na vibarua baba na mama lishe. Aidha, kukamilika kwa mradi huu kumebadilisha taswira nzima ya eneo la Magomeni na kuboresha muonekano wake na ustawi wa jamii.
16.Mheshimiwa Spika, hivi karibuni mradi wa ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje (Outer Ring Road) yenye urefu wa kilometa 112.3 katika Jiji la Dodoma umezinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan. Tayari Makandarasi wameanza ujenzi wa barabara hiyo ambayo itakuwa ni kichocheo cha ukuaji wa uchumi na kurahisisha usafirishaji wa mizigo inayotumia barabara za Ushoroba wa Kati. Vilevile, upanuzi kwa njia nane wa barabara ya Kimara - Kibaha(km 19.2) umeendelea kutekelezwa ambapo barabara hii ikikamilika itakuwa suluhisho la changamoto ya msongamano wa magari katika barabara ya Morogoro. Miradi mingine ya barabara ambayo iko hatua za ujenzi kwa kiwango cha lami kuanzia awamu ya sita ni pamoja na Mradi wa magari yaendayo kwa kasi awamu ya tatu katika jiji la Dar es Salaam (km 23.33) pamoja na vituo vya mabasi, barabara ya Tanga - Saadani-Bagamoyo (km 256 km) sehemu ya Mkange - Mkwaja Pangani (km 91.5) pamoja na Kipumbwi Spur (km 3.7), Malagarasi – Ilunde – Uvinza (km 51.1), Bugene - Kasulo (Benaco) - Kumunazi (km 128.5) sehemu ya Bugene - Burigi Chato National Park (km 60).
17.Mheshimiwa Spika, miradi mingine ya barabara ipatayo 22 imepata kibali cha kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami. Kati ya miradi hiyo, mikataba ya kazi za ujenzi ambayo imesainiwa niBarabara ya Ntendo – Muze – Kilyamatundu (km 179) sehemu ya Ntendo – Kizungu (km 25); Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti River – Lalago – Maswa (km 389) sehemu ya Mbulu – Garbabi (km 25); Matai – Kasesya (km 50.6 ); Tarime – Mugumu (km 87.14), sehemu ya Tarime – Nyamwaga (25);Mpanda –Mishamo – Uvinza - Kanyani (km 250.4) sehemu ya Vikonge – Luhafwe (km 25);Makongorosi – Rungwa – Itigi –Mkiwa, sehemu ya Noranga – Itigi (Mrongoji) (km 25); Handeni – Kibirashi– Kibaya– Kwa Mtoro – Singida (km 460) sehemu ya Handeni – Kwediboma (km 20); Kitai – Lituhi (km 85) pamoja na Daraja la Mnywamaji, sehemu ya Amanimakoro – Ruanda (km 35); Ntyuka Jct – Mvumi – Kikombo (km76) na Chololo –Mapinduzi (TPDF HQ (km 5) sehemu ya Ntyuka –Mvumi- Makuru (8.6) na Kikombo Jct – Chololo – Mapinduzi (TPDF HQ) (km 16.4); Kabaoni – Sitalike (km 74) sehemu ya Kibaoni –Mlele (km 50); Itoni – Ludewa – Manda (km 211.4) sehemu ya Itoni – Lusitu (km 50) naMianzini – Ngaramtoni (km 18).
Aidha, barabara nyingine ziko katika hatua ya manunuzi ya kupata makandarasi ambazo nibarabara ya TAMCO – Vikawe – Mapinga (km 24); Ibanda – Itungi (km 26); Omugakorongo – Kigarama – Murongo sehemu ya Murongo – Kigarama(km 50); Sengerema – Nyehunge – Kahunda sehemu ya Sengerema – Nyehunge (km 54); Nzera – Nkome (km 20); Same – Kisiwani – Mkomazi (km 97); Ubena Zomozi – Ngerengere (km 11.6); Ifakara – Kihansi (km 50); Kibada – Mwasonga – Tundwi Songani – Kimbiji (km 41); Uyole – Ifisi(km 29); Likuyufusi – Mkenda (sehemu ya Likuyufusi – Mhukuru km 60); Bigwa – Matombo – Mvuha (km 78); Isyonje – Kikondo – Makete (km 96.2) sehemu ya Ipelele – Iheme (km 25); Kibaoni – Sitalike (km 74) sehemu ya Mlele – Sitalike (km 24) na Kibondo – Mabamba (km 48).
18.Mheshimiwa Spika, kuhusu usafiri kwa njia ya reli, Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea na kazi za ujenzi wa reli ya SGR kwa awamu mbili, ambapo Serikali imeendelea na ujenzi wa awamu ya kwanza iliyogawanyika katika vipande vitano (5) kati ya Dar es Salaam na Mwanza. Utekelezaji wa ujenzi wa vipande hivyo umefikia katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Aidha, Serikali imeanza utekelezaji wa ujenzi wa reli ya SGR katika awamu ya pili kati ya Tabora na Kigoma ambapo fedha za utekelezaji huo zimeanza kutengwa katika mwaka wa fedha 2022/2023.
19.Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Sita imeonesha dhamira ya dhati ya kuboresha viwanja vya ndege ili kurahisisha upatikanaji wa huduma bora za usafiri na usafirishaji kwa njia ya anga.Katika kufanikisha hilo, ujenzi pamoja na uboreshaji wa viwanja vya ndege katika mikoa mbalimbali nchini umeendelea kutekelezwa. Miradihiyo ni pamoja na ujenzi na ukarabati wa Viwanja vya Ndege vya Songea, Mtwara, Iringa, Musoma na Songwe.Vilevile, mkataba wa Awamu ya Kwanza ya ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato Mkoani Dodoma umesainiwa na Mkandarasi yupo katika hatua za maandalizi ya kuanza ujenzi. Aidha, kuhusu Awamu ya Pili ya ujenzi wa Jengo la Abiria na Miundombinu yake katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato, tayari Serikali imesaini mkataba wa ujenzi. Sanjari na kuboresha viwanja vya ndege, Serikali imeendelea kuboresha Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) ambapo katika kipindi cha miezi tisa iliyopita, ATCL imepokea ndege tatu (3) ambapo kati ya hizo ndege mbili (2) ni za masafa ya kati na ndege moja (1) ni ya masafa mafupi.
20.Mheshimiwa Spika, kuhusu upanuzi na uboreshaji wa Bandari ya Dar es Salaam, Serikali imekamilisha ujenzi wa Gati la kushusha magari (RORO) pamoja na kuboresha Gati Namba 1 hadi 7 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, MheshimiwaSamia Suluhu Hassan alizindua miradi hii tarehe 04 Disemba, 2021. Matokeo ya ujenzi na maboresho haya yameanza kuonekana ambapo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania imefanikiwa kuhudumia meli kubwa ya magari katika historia yake ikiwa imeshusha magari 4,397 tarehe 09 Mei, 2022. Hii imewezekana kutokana na maboresho yaliyofanywa kwenye Bandari ya Dar es Salaam.
21.Mheshimiwa Spika, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) imewezesha upatikanaji wa karakana sita zinazotembea na hivyo kufikia saba kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa matengenezo ya magari katika maeneo yasiyofikia kwa urahisi. Karakana hizo zinahudumia maeneo ya pembezoni katika mikoa ya Pwani, Arusha, Mbeya, Dodoma, Mwanza, Tabora na Mtwara. Vilevile, Wizara imefunga Mfumo wa Kielektroniki wa Kukusanya Mapato (N – Card) katika kituo cha Magogoni – Kigamboni mwezi Machi, 2022. Kwa sasa watumiaji wa kivuko hiki wanatumia kadi maalum kulipia tozo kwa ajili ya kuvuka badala ya tiketi zilizokuwa zikitumika awali. Ni matarajio ya Serikali kuwa Mfumo huu utaboresha ukusanyaji wa maduhuli ya Serikali.
C. MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA WIZARA NA TAASISI ZAKE KWA MWAKA WA FEDHA 2021/22
22.Mheshimiwa Spika, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imegawanywa katika mafungu mawili ya kibajeti: Fungu 62 (Sekta ya Uchukuzi) na Fungu 98 (Sekta ya Ujenzi). Nitaanza na maelezo kuhusu utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2021/22 kwa Sekta ya Ujenzi ikifuatiwa na Sekta ya Uchukuzi.
C.1SEKTA YA UJENZI
Bajeti ya Matumizi ya Kawaida
23.Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/22, Sekta ya Ujenzi ilitengewa jumla ya Shilingi 38,540,787,000.00kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo, Shilingi 35,186,389,000.00 ni kwa ajili ya Mishahara ya Watumishi wa Wizara na Taasisi zake na Shilingi 3,354,398,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo ya Wizara na Taasisi zake.
Hadi Aprili, 2022 jumla ya Shilingi 31,578,893,459.84, sawa na asilimia 81.94 ya fedha zilizoidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilikuwa zimetolewa na HAZINA kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo, Shilingi 29,092,402,936.04 ni kwa ajili ya Mishahara ya Watumishi wa Wizara na Taasisi na Shilingi 2,486,490,523.80 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo ya Wizara na Taasisi zake.
Bajeti ya Miradi ya Maendeleo
24.Mheshimiwa Spika, kwa upande wa miradi ya maendeleo, katika mwaka wa fedha 2021/22, Sekta ya Ujenzi ilitengewa Shilingi 1,588,703,487,200.00. Kiasi hicho kinajumuisha Shilingi 1,288,703,487,200.00 fedha za ndani na Shilingi 300,000,000,000.00 fedha za nje. Fedha za ndani zilijumuisha fedha za Mfuko Mkuu wa Serikali (Consolidated Funds) ambazo ni Shilingi 652,854,360,000.00 na fedha za Mfuko wa Barabara ni Shilingi 635,849,127,200.00.
Hadi Aprili, 2022 fedha zilizopokelewa ni Shilingi 1,532,703,487,200.00 sawa na asilimia 96.48 ya fedha zilizoidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2021/22. Kati ya fedha hizo, Shilingi 1,232,741,391,541.94 ni fedha za ndani na Shilingi 299,962,095,658.06ni fedha za nje. Fedha za ndani zilizopokelewa zinajumuisha Shilingi 691,100,092,642.94 kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali na Shilingi 541,641,298,899.00 kutoka Mfuko wa Barabara.
UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO
Miradi ya Barabara na Madaraja
25.Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/22, Wizara yangu kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) ilipanga kutekeleza miradi ya barabara kuu inayohusisha ujenzi wa barabara zenye urefu wakilometa 467.11 kwa kiwango cha lami, ujenzi wa madaraja 14 pamoja na ukarabati wa kilometa 32.47 kwa kiwango cha lami katika barabara kuu.
Hadi kufikia Aprili, 2022ujenzi wa kilometa 216.26 za barabara kuu kwa kiwango cha lami umekamilika, sawa na asilimia 46 na ukarabati wa kilometa 2.5 sawa na asilimia 8 za Barabara Kuu. Aidha, utekelezaji wa miradi ya madaraja ya Kiyegeya (Morogoro), Daraja Jipya la Selander mkoani Dar es Salaam, Kitengule mkoani Kagera na Ruhuhu mkoani Ruvuma umekamilika na madaraja mengine yapo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
26.Mheshimiwa Spika, kwa upande wa barabara za mikoa, Wizara kupitia TANROADS ilipanga kujenga kwa kiwango cha lami jumla ya kilometa 103.0 ambapo kilometa 72.2 zilipangwa kujengwa kwa kutumia fedha za Mfuko Mkuu wa Serikali na kilometa 30.8 zilipangwa kujengwa kwa fedha za Mfuko wa Barabara. Kazi nyingine ni ukarabati kwa kiwango cha changarawe jumla ya kilometa 1,124.3. Kati ya hizo, kilometa 698.3 pamoja na madaraja/makalavati 34 yalipangwa kukarabatiwa kwa kutumia fedha za Mfuko Mkuu wa Serikali na kilometa 426 pamoja na madaraja/ makalavati 32 yalipangwa kujengwa/kukarabatiwa kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara.
Hadi Aprili, 2022 jumla ya kilometa 34.8 za barabara za mikoa zilijengwa kwa kiwango cha lami na jumla ya kilometa 307.41zilikarabatiwa kwa kiwango cha changarawe. Aidha, utekelezaji wa miradi ya madaraja upo katika hatua mbalimbali. Utekelezaji wa miradiuliathiriwa kwa kuchelewa kupatikana kwa misamaha ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT). Hata hivyo, Wizara ya Fedha na Mipango kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeandaa Mfumo wa Kielektroniki utakaorahisisha upatikanaji wa misamaha ya kodi.
27. Mheshimiwa Spika,Wizara vilevile ilipanga kufanya matengenezo ya kawaida (routine and recurrent maintenance) kwa kilometa 33,171.89, matengenezo ya muda maalum kilometa 4,783.72 matengenezo ya sehemu korofi kilometa 549.38 pamoja na matengenezo ya madaraja 3,291 katika barabara kuu na barabara za mikoa. Kazi nyingine ni shughuli za udhibiti wa uzito wa magari na eneo la hifadhi za barabara na mradi wa matengenezo ya barabara kwa mikataba ya muda mrefu.
Hadi Aprili, 2022 mpango wa matengenezo katika barabara kuu na za mikoa ulikuwa umekamilika kwa asilimia 30. Aidha, jumla ya magari 3,821,559 yalikuwa yamepimwa katika vituo 66 vya mizani iliyopo nchini ambapo kati ya hayo, magari31,055 sawa na asilimia 0.82 yalikuwa yamezidisha uzito zaidi ya asilimia 5 ya uzito unaoruhusiwa. Jumla ya Shilingibilioni 2.97 zilikusanywa kutokana na tozo ya uharibifu wa barabara. Ili kuongeza uwazi na uwajibikaji na kupunguza vitendo vya rushwa kwenye mizani, Wizara kupitia TANROADS imeweka mifumo ya kamera (CCTV) katika mizani 13 na itaendelea kuweka katika mizani nyingine. Vilevile, Wizara inaendelea na utoaji wa vibali vya usafirishaji barabarani wa mizigo maalum nchini kwa kutumia mfumo ujulikanao Special Load Permit System.
28.Mheshimiwa Spika, hadi Aprili, 2022 jumla ya vibali 35,818 vilitolewa na jumla ya Shilingi bilioni 12.80 zilikusanywa kutokana na tozo ya upitishaji wa mizigo maalum. Vilevile, mvua kubwa zilizonyesha nchini kuanzia Novemba, 2021 hadi Februari, 2022 zilisababisha uharibifu mkubwa wa barabara katika mikoa 14 ambayo ni Arusha, Dodoma, Mbeya, Morogoro, Ruvuma, Pwani, Dar es Salaam, Iringa, Manyara, Katavi, Singida, Tanga na Kilimanjaro. Matengenezo ya barabara hizo yalifanyika na kukamilika.
29.Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa miradi ya barabara kwa mwaka 2021/22 hadi kufikia Aprili, 2022 ni kama ifuatavyo:
30.Mheshimiwa Spika, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Barabara ya Soni – Bumbuli – Dindira – Korogwe (km 74) inaendelea.
31.Mheshimiwa Spika, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Barabara ya Mtwara – Newala – Masasi (km 210) umekamilika. Aidha, Serikali imekamilisha ujenzi wa sehemu ya Mtwara – Mnivata (km 50).Mkataba wa ufadhili kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa sehemu iliyobaki ya Mnivata – Tandahimba – Newala – Masasi (km160) umesainiwa. Kwa sasa nyaraka za zabuni zimewasilishwa AfDB kwa ajili ya kupata kibali cha kutangaza (No Objection).
32.Mheshimiwa Spika, kwa Barabara ya Likuyufusi – Mkenda (km 122.50), hadi kufikia Aprili, 2022, Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina umekamilika. Taratibu za kutangaza zabuni za ujenzi wa barabara hii sehemu ya Likuyufusi – Mhukuru (km 60) zinaendelea.
33.Mheshimiwa Spika, kuhusu mradi wa ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Nachingwea – Liwale (km 130), hadi kufikia Aprili, 2022, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina umekamilika.
34.Mheshimiwa Spika, kwa Barabara ya Ubena Zomozi – Ngerengere (km 11), hadi Aprili, 2022, usanifu wa kina umekamilika na zabuni za kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa barabara hii zimetangazwa.
35.Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Barabara ya TAMCO – Vikawe – Mapinga (km 24), taratibu za manunuzi kwa ajili ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami zinaendelea.
36.Mheshimiwa Spika, kazi za upembuzi yakinifu na usanifu wa kinawa Barabara ya Makofia – Mlandizi (km 36.7) zimekamilika. Serikali inaendelea kutafuta fedha za ujenzi.
37.Mheshimiwa Spika, kwa Barabara ya Musoma – Makojo – Busekela (km 92), hadi kufikia Aprili, 2022, ujenzi wa barabara hii unaendelea kwa sehemu ya Suguti – Kusenyi (km 5) ambapo umefikia asilimia 74.
38.Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Barabara ya Kongwa Jct – Mpwapwa – Gulwe – Kibakwe(km98) unafanyika kwa awamu. Hadi Aprili, 2022, ujenzi wa kilometa 5.8 umekamilika na ujenzi wa kilometa tatu (3) unaendelea na umefikia asilimia 20.
39.Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Barabara ya Muhutwe – Kamachumu – Muleba (km 54) unafanyika kwa awamu. Hadi Aprili, 2022, mradi huu unaendelea na kilometa 29 zimekamilika kwa kiwango cha lami. Aidha, ujenzi wa kilometa 6.5 kwa kiwango cha lami unaendelea na umefikia asilimia 30.
40.Mheshimiwa Spika, kuhusu ujenzi waBarabara ya Iringa – Ruaha National Park (km 104), taratibu za kusaini makubaliano yamkopo kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami zinaendelea.
41.Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Barabara ya Muheza – Amani (km 36) unafanyika kwa awamu. Hadi Aprili, 2022, kazi za ujenzi wa kilometa 7 zinaendelea na zimefikia asilimia 98.
42.Mheshimiwa Spika, kuhusu mradi wa ukarabati kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Mtwara – Mingoyo – Masasi (km 200), hadi kufikia Aprili, 2022, taratibu za kupata fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kugharamia ukarabati wa barabara hii zinaendelea.
43.Mheshimiwa Spika, kwa Barabara ya Kibaoni – Majimoto – Muze – Kilyamatundu (km 189) hadi kufikia Aprili, 2022, kazi za upembuzi yakinifu na usanifu wa kina zimekamilika kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Kibaoni – Majimoto – Inyonga (km 152) na Ntendo – Muze – Kilyamatundu (km 200) kwa kiwango cha lami. Aidha, mkataba kwa ajili ya ujenzi wasehemu ya Ntendo – Kizungu (km 25) umesainiwa Machi, 2022. Vilevile, taratibu za manunuzi kwa ajili ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa sehemu ya Kizungu – Muze (km 12) zinaendelea.
44.Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Daraja la Kigongo – Busisi (J.P. Magufuli) na Barabara Unganishi unaendeleana hadi Aprili, 2022, mradi umefikia asilimia 40.18.Aidha, hadi Aprili, 2022 ujenzi wa Daraja la Kitengule na Barabara Unganishi (km 18) umekamilika na kazi ya ujenzi wa barabara unganishi inaendelea na kwa ujumla mradi umefikia asilimia 73.89. Kuhusu Daraja Jipya la Wami, kazi za ujenzi zinaendelea na zimefikia asilimia 72.88. Vilevile, usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Mzinga na Daraja la Ugalla, umekamilika. Serikali inaendelea kutafuta fedha za ujenzi wa madaraja haya.
45.Mheshimiwa Spika,kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Barabara ya Morogoro – Dodoma Pamoja na Daraja la Mkundi inaendelea. Aidha, katika mradi waBarabara ya Njombe – Makete – Isyonje (km 157.4), hadi kufikia Aprili, 2022, ujenzi wa sehemu ya barabara ya Njombe – Moronga (km 53.9) kwa kiwango cha lami umekamilika naujenzi wa sehemu ya Moronga – Makete (km 53.5) umefikia asilimia 85. Vilevile, taratibu za manunuzi ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa kilometa 25 za sehemu ya Isyonje – Makete (km 50) zinaendelea ambapo zabuni zimefunguliwa tarehe 22 Aprili, 2022 na tathmini ya zabuni inaendelea.
46.Mheshimiwa Spika, kuhusu Barabara ya Omugakorongo – Kigarama – Murongo (km 105), hadi kufikia Aprili, 2022 mradi huu uko katika hatua za manunuzi ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi.
47.Mheshimiwa Spika, kwa Barabara ya Nanganga – Ruangwa – Nachingwea (km 145), hadi kufikia Aprili, 2022 ujenzi kwa kiwango cha lami wa sehemu ya Nanganga – Ruangwa (km 53.2) umefikia asilimia 42. Aidha, Serikali inaendelea kutafuta fedha za ujenzi wa sehemu ya Masasi – Nachingwea (km 45) na sehemu ya Ruangwa – Nachingwea (km 47).
48.Mheshimiwa Spika, kuhusu Barabara ya Mpemba – Isongole, hadi kufikia Aprili 2022, ujenzi kwa kiwango cha lami wa sehemu ya Mpemba – Isongole (km 51.2) ulikuwa umekamilika na ujenzi wa daraja la Songwe unaendelea. Aidha, kazi ya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa kinainaendelea ikiwa ni hatua za maandalizi ya ujenzi wa sehemu ya Ruanda – Iyula – Nyimbili (km 21) na Katumbasongwe – Kasumulu – Ngana – Ileje (km 90.1) kwa kiwango cha lami.
49.Mheshimiwa Spika, katika Barabara ya Tanga – Pangani – Makurunge (km 174.5), hadi kufikia Mei, 2022 ujenzi wa sehemu ya Tanga – Pangani (km 50) unaendelea na umefikia asilimia 37. Aidha, mkataba wa ujenzi wa barabara ya Pangani – Mkange (km 124.5) sehemu ya Tungamaa – Mkange (km 98.9) na ujenzi wa Daraja la Panganiumesainiwa na Mkandarasi yupo kwenye maandalizi ya kuanza ujenzi.
50.Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Barabara ya Kisarawe – Maneromango (km 54) unafanyika kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Hadi Aprili 2022, kilometa 20.1 zimekamilika naujenzi wa kilometa 3.3 unaendelea.
51.Mheshimiwa Spika, kuhusu Barabara ya Geita – Bulyanhulu – Kahama (km 174), hadi kufikia Aprili 2022, maandalizi ya kuanza ujenzi wa sehemu ya Geita – Bulyanhulu Jct (km 58.3), Bulyanhulu Jct – Kahama (km 61.7) na Uyogo – Nyamilangano – Nyandekwa – Kahama (km 54) yanaendelea.
52.Mheshimiwa Spika, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Barabara ya Nyamirembe Port – Katoke (km 50) imekamilika na Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii. Aidha, upembuzi yakinifu na Usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa sehemu ya SIDO – Chato Zonal Hospital (km 5.3) na Chato Ginery – Bwina (km 8.1) umekamilika. Vilevile, taratibu za kumpata Mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa Barabara ya Geita – Nzera(km 54) kwa kiwango cha lami zinaendelea.
53.Mheshimiwa Spika, kwa mradi wa Barabara ya Arusha – Moshi – Himo – Holili (km 199.51), hadi kufikia Aprili 2022, ujenzi wa sehemu ya Sakina – Tengeru na Barabara ya Mchepuo ya Arusha (km 56.51) ulikuwa umekamilika.Vilevile, ujenzi wa barabara ya Kijenge – Usa River (Nelson Mandela AIST) (km 20) unaendelea. Aidha, Mkataba wa ujenzi wa barabara ya Mianzini – Ngaramtoni (km 18) kwa kiwango cha lami umesainiwa na kwa sasa Mkandarasi yupo kwenye hatua za maandalizi ya kuanza ujenzi.
Kwa sehemu ya Tengeru – Moshi – Himo na Mizani ya Himo (km 105), tayari Serikali ya Tanzania na Serikali ya Japan zimesaini makubaliano ya mkopo kwa ajili ya upanuzi wa sehemu ya Tengeru – Usa River (km 9.3). Mkopo huo utahusisha pia ujenzi wa Daraja la Kikafu (mita 560) na barabara unganishi (km 3.5) pamoja na ujenzi wa barabara sehemu ya Moshi Mjini (km 8.4).Taratibu za manunuzi kwa ajili ya kumpata Mhandisi Mshauri kwa ajili ya usimamizi wa ujenzi zinaendelea.
54.Mheshimiwa Spika, katika mradi wa ujenzi wa Barabara za Kuelekea Kwenye Mradi wa Kufua Umeme Katika Maporomoko ya Mto Rufiji (Access Roads to Rufiji Hydropower Project), hadi Aprili, 2022, ujenzi wa barabara yote yaBigwa – Matombo – Mvuha (km 78) kwa kiwango cha lami upo katika hatua za manunuzi ya kumpata Mkandarasi.Aidha, taratibu za manunuzi ya Mhandisi Mshauri wa kufanya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Ubena Zomozi – Mvuha – Kisaki – Mtemele Jct (km 178) kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami zinaendelea.Vilevile, ukarabati kwa kiwango cha changarawe wa barabara ya Maneromango – Vikumburu – Mloka (km 100) na Kibiti – Mloka – Mtemele – Rufiji (km 203) unaendelea.
55.Mheshimiwa Spika, kuhusu Barabara ya Dar es Salaam – Chalinze – Morogoro – Dodoma (km 152.30), hadi kufikia Aprili 2022, kazi ya kubainisha itakapopita barabara mpya pamoja na uthamini wa mali zitakazoathirika kwa ajili ya kulipa fidia katika sehemu ya Kibaha - Mlandizi – Chalinze – Morogoro Expressway (km 158) inaendelea. Kwa sehemu ya Mlandizi – Chalinze (km 44), kazi ya ukarabati inaendelea.Aidha, ujenzi wa barabara ya Kwa Mathias (Morogoro Road) – Msangani (km 8.3) unaendelea ambapo kilometa 2.95 zimekamilika na mita 400 zinaendelea kujengwa. Vilevile, kazi ya maboresho ya maeneo hatarishi (blackspots) katika mikoa ya Pwani na Morogoro imekamilika.
56.Mheshimiwa Spika, kwa Barabara ya Wazo Hill – Bagamoyo – Msata (km 118.10) kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina imekamilika. Serikali inaendelea kutafuta fedha za ukarabati wa sehemu ya Tegeta – Bagamoyo (km 46.9) na ujenzi wa barabara ya Mbegani – Bagamoyo (km 7.2) kwa kiwango cha lami.
57.Mheshimiwa Spika, katika Barabara ya Usagara – Geita – Buzirayombo – Kyamyorwa (km 110), kazi za ujenzi zimekamilika kwa barabara ya Uyovu – Bwanga – Biharamulo (Lot 1 and Lot 2) (km 110). Aidha, Serikali inaendelea kutafuta fedha za ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Nyakahura – Kumubuga – Rulenge – Kabanga Nickel (km 141) kwa sehemu ya Rulenge – Kabanga Nickel (km 32), Kumubuga –Rulenge – Murusagamba (km 75) na Nyakahura – Kumubuga – Murusagamba (km 34).
58.Mheshimiwa Spika, katika Barabara ya Kigoma – Kidahwe – Uvinza – Kaliua – Tabora (km 389.7), miradi iliyokamilika ni ujenzi wa Daraja la Kikwete (Malagarasi), Kidahwe – Uvinza (km 76.6), Tabora – Ndono (km 42), Ndono – Urambo (km 51.98), Kaliua – Kazilambwa (km 56) na Urambo – Kaliua (km 28). Aidha, hadi Aprili, 2022 ujenzi wa sehemu ya Kazilambwa – Chagu (km 36) umefikia asilimia 32.5 na ujenzi wa sehemu ya Uvinza – Malagarasi (km 51.1) unaendelea.
59.Mheshimiwa Spika,katika Barabara ya Ifakara – Kihansi – Mlimba – Madeke – Kibena (km 270), taratibu za manunuzi kwa ajili ya kumpata Mhandisi Mshauri wa kufanya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa sehemu ya Kihansi – Mlimba – Taweta -Madeke –Lupembe - Kibena (km 220) kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) zipo katika hatua za mwisho kukamilika. Aidha, taratibu za manunuzi kwa ajili ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa sehemu ya Ifakara – Kihansi (km 50)zinaendelea.
60.Mheshimiwa Spika, katika Barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti River – Lalago – Maswa (km 389), mradi upo katika hatua za majadiliano ya kimkataba kwa ajili ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa kilometa 25 za sehemu ya Mbulu –Garbabi. Aidha, taratibu za kumpata Mkandarasi wa sehemu ya Garbabi – Haydom (km 25) zinaendelea. Kuhusu Barabara ya Marangu – Tarakea – Rongai – Kamwanga /Bomang’ombe – Sanya Juu (km 84.80), kazi za ujenzi zimekamilika kwa sehemu ya Sanya Juu – Alerai (km 32.2) na KIA – Mererani (km 26). Aidha, kilometa 14.75 za ujenzi kwa kiwango cha lami kwa sehemu ya Kwa Sadala – Masama – Machame Junction (km 16) zimekamilika na mita 350 zinaendelea kujengwa. Kwa upande wa barabara ya Kiboroloni – Kiharara – Tsuduni – Kidia (km 10.8) ujenzi umekamilika kwa kilometa 3.07 na kilometa 1.9 zinaendelea kujengwa. Aidha, Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Tarakea – Holili (km 53) unaendelea.
61.Mheshimiwa Spika, katika Barabara ya Tukuyu – Mbambo – Katumba (km 60.6), ujenzi wa sehemu ya Bujesi – Mbambo (km 26) na Tukuyu – Mbambo (km 34.6) unaendelea ambapo hadi Aprili, 2022 ulifikia asilimia 60. Aidha, kazi za upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa sehemu ya Mbambo – Ipinda (km 19.7) zinaendelea.
62.Mheshimiwa Spika, mradi wa Barabara ya Dodoma – Manyoni (km 127) na Barabara ya Mchepuo Kuingia Manyoni Mjini (km 4.8) unahusisha ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Ukaguzi (One Stop Inspection Station – OSIS) cha Muhalala (Manyoni). Mkataba wa awali wa utekelezaji wa mradi huu umesitishwa kutokana na changamoto za kimkataba ambapo utekelezaji wake ulikuwa umefikia asilimia 50. Taratibu za kumpata Mkandarasi mpya wa kumalizia kazi hizo zinaendelea.
63.Mheshimiwa Spika, maandalizi ya ujenzi wa Barabara ya Tabora – Mambali – Bukene – Itobo (km 114) yanaendelea. Aidha, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Barabara ya Namanyere – Katongoro – New Kipili Port (km 64.8) imekamilika. Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii.
64.Mheshimiwa Spika,katika Barabara ya Dumila – Kilosa – Mikumi (km 119), ujenzi wa sehemu ya Rudewa – Kilosa (km 24) unaedelea na umefikia asilimia 84.35. Aidha, maandalizi ya ujenzi wa sehemu ya Kilosa – Ulaya – Mikumi (km 72) kwa kiwango cha lami yanaendelea.
65.Mheshimiwa Spika, kuhusu Barabara ya Sumbawanga – Matai – Kasanga Port (km 162), ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami umekamilika. Aidha, ujenzi wa barabara ya Matai – Kasesya (km 50 ) sehemu ya Matai – Tatanda (km 25) upo katika hatua ya kusaini mkataba na sehemu iliyobaki ya Tatanda – Kasesya (km 25) ipo katika hatua za manunuzi kwa ajili ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi.
66.Mheshimiwa Spika, kuhusu Ujenzi wa Madaraja Makubwa miradi iliyotengewa fedha kwa mwaka 2021/22 iliyokamilika ni ujenzi wa Daraja la Tanzanite (Dar es Salaam), Daraja la Sibiti (Singida), Daraja la Kiyegeya (Morogoro), Daraja la Magufuli (Morogoro), Daraja la Ruhuhu (Ruvuma), Daraja la Momba (Rukwa), Daraja la Mlalakuwa (Dar es Salaam), Daraja la Magara (Manyara), Daraja la Lukuledi (Lindi) na Daraja la Mara. Miradi mingine iliyokamilika ni Usanifu wa kina wa daraja la Simiyu (Mwanza), Daraja la Mitomoni (Ruvuma), Daraja la Godegode (Dodoma), Daraja la Sukuma (Mwanza), Daraja la Mkenda (Ruvuma), Daraja la Sanza (Singida) na Daraja la Mtera (Dodoma).
Kazi zinazoendelea ni ujenzi wa Daraja la Msingi (Singida) ambalo utekelezaji wake umefikia asilimia 81 na ununuzi wa Madaraja ya Chuma (Steel Bridges Emergency Parts) uko katika hatua za mwisho. Aidha, kazi ya usanifu wa kina wa Daraja la Malagarasi Chini (Kigoma) inaendelea. Kuhusu ujenzi wa barabara unganishi katika Daraja la Sibiti (Singida), taratibu za manunuzi ya kumpata Mkandarasi zinaendelea.
67.Mheshimiwa Spika, kuhusu mradi wa Barabara ya New Bagamoyo (Kawawa Jct – Tegeta km 18.3) kazi za upanuzi wa sehemuya Morocco – Mwenge (km 4.3) zimekamilika.
68.Mheshimiwa Spika, kuhusu Barabara ya Kyaka – Bugene – Kasulo (km 222.10), ujenzi wa sehemu ya Kyaka – Bugene (km 59.1) ikijumuisha ujenzi wa Daraja la Mwisa umekamilika. Aidha, mkataba wa ujenzi wa barabara ya Bugene – Kasulo –Kumunazi & Kyaka – Mutukula (km 163) sehemu ya Bugene – Burigi Chato National Park (km 60) umesainiwa na Mkandarasi yupo katika hatua za maandalizi ya kuanza ujenzi. Katika barabara ya Murushaka – Nkwenda – Murongo (km 125); hadi kufikia Aprili, 2022 zabuni za ujenzi wa sehemu Kyerwa – Chonyonyo (km 50) zimetangazwa. Aidha, taratibu za manunuzi kwa ajili ya kumpata Mhandisi Mshauri wa kufanya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina kwa sehemu iliyobaki yenye urefu wa kilometa 75 zinaendelea.
69.Mheshimiwa Spika, katika mradi wa Barabara ya Isaka – Lusahunga (km 242.2), kazi za ukarabati wa sehemu yaIsaka – Ushirombo (km 132.2) na Ushirombo – Lusahunga (km 110) zimekamilika. Aidha, manunuzi ya kumpata Mkandarasi kwa ajili ya ukarabati kwa kiwango cha lami wa sehemu yaLusahunga – Rusumo (km 92) yapo katika hatua ya mwisho. Kwa upande wa ujenzi wa Kituo cha Ukaguzi cha Nyakanazi, mkataba wa awali umesitishwa kutokana na changamoto za kimkataba. Taratibu za kumpata Mkandarasi mpya wa kumalizia kazi hizo zinaendelea.
70.Mheshimiwa Spika, kuhusu Barabara ya Manyoni – Itigi – Tabora (km 259.7) ujenzi wa barabara umekamilika kwa sehemu ya Tabora – Nyahua (km 85), Nyahua – Chaya (km 85.4) na Manyoni – Itigi – Chaya (km 89.35).
71.Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/22, kazi zilizopangwa kutekelezwa kwa ajili ya miradi ya Barabara za Mikoani kilometa 770.5 na ujenzi wa madaraja 34.Kati ya hizo, kilometa 698.3zilipangwa kukarabatiwa kwa kiwango cha changarawe na kilometa72.2 kujengwa kwa kiwango cha lami.
Hadi kufikia Aprili 2022, kilometa 307.41 sawa na asilimia 44.02 ya malengo ya barabara za mikoa zilikuwa zimekarabatiwa kwa kiwango cha changarawe na kilometa 34.8 sawa na asilimia 48.19 ya lengo, zimejengwa kwa kiwango cha lami. Aidha, ujenzi wa madaraja ulikamilika kwa asilimia 6.42.
72.Mheshimiwa Spika, hadi kufikia Aprili 2022, kazi za upembuzi yakinifu na usanifu wa kina zinaendelea kwa ajili ya ukarabati wa Barabara ya Mwanza/Shinyanga Border – Mwanza (km 102) kwa kiwango cha lami.
73.Mheshimiwa Spika, katika mradi wa barabara za kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam, hadi Aprili, 2022 miradi iliyokamilika ni ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara za Mbezi – Malambamawili – Kinyerezi – Banana (km14), Tegeta - Kibaoni - Wazo Hill - Goba - Mbezi (km 20) sehemu ya Mbezi Mwisho – Goba,Tangi Bovu – Goba (km 9), Kimara Baruti –Msewe – Changanyikeni (km 2.6), Banana – Kitunda – Kivule – Msongola, (km 14.7) sehemu ya Kitunda– Kivule (km 3.2), Ardhi – Makongo – Goba (sehemu ya Goba – Makongo km 4) na Tegeta Kibaoni – Wazo Hill – Goba – Mbezi/Morogoro Road (sehemu ya Mbezi Mwisho – Goba km 7), Wazo Hill – Madale (km 9) na Wazo Hill (Madale) – Goba (km 5).
Mradi unaoendelea kutekelezwa ni ujenzi wa barabara ya Ardhi – Makongo – Goba (sehemu ya Ardhi – Makongo km 5) ambao hadi Aprili, 2022 umefikia asilimia 84. Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradiwa upanuzi wabarabara ya Mwai Kibaki (km 9),Mjimwema – Kimbiji – Pembamnazi (km 27), Kongowe – Mjimwema – Kivukoni Ferry (km 25.1), Kibamba – Kisopwa – Kwembe – Makondeko (km 14.66) sehemu ya Mloganzila – Mloganzila Citizen (km 4) na Goba - Matosa – Temboni (km 6).
74.Mheshimiwa Spika, katika Barabara ya Nyamuswa – Bunda – Kisorya (km 106), ujenzi wa barabara ya Kisorya – Bulamba (km 51) umekamilika na ujenzi wa barabara ya Nyamuswa – Bunda – Bulamba (km 56.4) unaendelea na umefikia asilimia 35. Vilevile, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Barabara ya Kolandoto – Lalago – Ng’oboko - Mwanhuzi (km 122) umekamilika na barabara hii itajengwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Hadi kufikia Aprili 2022, taratibu za manunuzi kwa ajili ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa Daraja la Itembe kwenye barabara hii zinaendelea.
75.Mheshimiwa Spika, ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Ndundu – Somanga (km 60) umekamilika. Aidha, Serikali inaendelea na maandalizi ya ukarabati wa sehemu za Kongowe – Ndundu (km 160.65) na Nangurukuru – Mbwemkuru (km 95).
76.Mheshimiwa Spika,hadi Aprili 2022, utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Barabara ya Kasulu – Manyovu pamoja na barabara za kuingia Kasulu Mjini (km 68) ulikuwa unaendelea na umefikia asilimia 18.
77.Mheshimiwa Spika, kuhusu mradi wa Barabara ya Mzunguko katika Jiji la Dodoma City Outer Dual Carriageway Ring Road Lot1 & 2 (km 112.3), ujenzi wa sehemu ya Nala – Veyula – Mtumba – Ihumwa Dry Port (km 52.3) unaendelea na umefikia asilimia 2.23 na ujenzi wa sehemu ya Ihumwa Dry Port – Matumbulu – Nala (km 60) umefikia asilimia 3.
Kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Makulu Jct. – Ntyuka R/About – Image R/About – Bahi R/About (km 6.3) imekamilika. Taratibu za kukamilisha mkopo wa mradi huu kutoka Serikali ya Japan zinaendelea. Aidha,mkataba wa ujenzi wa barabara ya Ntyuka Jct – Mvumi - Kikombo Jct. (km 76.07) na Chololo – Mapinduzi (JWTZ HQ) (km 5) sehemu ya Ntyuka Jct. – Ng’ong’ona Jct (km 8.6) na sehemu ya Kikombo Jct – Chololo – Mapinduzi (TPDF HQ) (km 16.4) umesainiwa na Mkandarasi yupo katika hatua za kuanza ujenzi. Vilevile, taratibu za kumpata Mhandisi Mshauri atakayefanya kazi ya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina kwa ajili ya Upanuzi wa Barabara Kuu zinazoingia Katikati ya Jiji la Dodoma (km 220) zipo katika hatua ya mwisho.
78.Mheshimiwa Spika, kuhusu barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupiro – Malinyi – Londo – Lumecha/Songea (km 512), hadi Aprili 2022, kazi za ujenzi kwa sehemu ya Kidatu – Ifakara (km 66.9) zilikuwa zinaendelea na zimefikia asilimia 51.1. Aidha, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa sehemu ya Ifakara – Lupiro – Malinyi – Londo – Lumecha/Songea (km 396) umekamilika na Serikali inaendelea kutafuta fedha za ujenzi.
79.Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Barabara ya Tabora – Ipole – Koga – Mpanda (km 383) umekamilika. Mradi huu ulihusisha ujenzi wa sehemu ya Usesula – Komanga (km 115),Komanga – Kasinde (km 120), Tabora – Sikonge (Usesula) (km 30) na Kasinde – Mpanda (km 118).
80.Mheshimiwa Spika, katika Barabara ya Makutano – Natta – Mugumu/Loliondo – Mto wa Mbu (km 235), hadi Aprili 2022, kazi za ujenzi wa barabara ya Makutano – Natta (Sanzate) (km 50) zilikuwa zimefikia asilimia 94 na kwa sehemu ya Sanzate – Natta (km 40) ujenzi umefikia asilimia 11.Aidha, kazi za ujenzi kwa barabara ya Loliondo – Mto wa Mbu (km 213); Sehemu ya Waso – Sale (km 50) zimefikia asilimia 97.36 na maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Natta – Mugumu (km 45)yanaendelea. Vilevile, mkataba wa ujenzi wa kwa kiwango cha lami wa barabara ya Tarime – Mugumu (km 86): sehemu ya Tarime – Nyamwaga (km 25) umesainiwa na Mkandarasi yupo katika hatua za maandalizi ya kuanza ujenzi. Aidha, taratibu za manunuzi kwa ajili ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa sehemu ya Nyamwaga – Mugumu (km 61) zinaendelea.
81.Mheshimiwa Spika, katika Barabara ya Ibanda – Itungi Port/Kajunjumele – Kiwira Port (km 66.6), taratibu za kumpata Mkandarasi wa ujenzi kwa kiwango cha lami wa sehemu ya Ibanda – Itungi Port (km 26) zinaendelea. Aidha, kazi za ujenzi wa sehemu ya Kikusya – Ipinda – Matema (km 39.1) zimekamilika na ukarabati wa barabara ya Uyole – Kasumulu, sehemu ya Ilima Escarpment (km 3) zimefikia asilimia 95. Maandalizi ya ujenzi wa sehemu ya Kajunjumele (Iponjola) – Kiwira Port (km 6) yanaendelea na ujenzi wa Kasumulu/ Songwe – Tanzania/Malawi Border OSBP unaendelea na umefikia asilimia 80.
82.Mheshimiwa Spika, katika Barabara ya Nzega – Tabora (km 289.7), ujenzi wa sehemu ya Nzega – Puge (km 58.6) na Puge – Tabora (km 56.1) umekamilika. Maandalizi ya ujenzi wa sehemu ya Nzega – Kagongwa (km 65) yanaendelea na mkataba wa kufanya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina kwa ajili ya ukarabati wa sehemu ya Shelui – Nzega (km 110) umesainiwa.
83.Mheshimiwa Spika, kuhusu Barabara ya Sumbawanga – Mpanda – Nyakanazi (km 541.5), ujenzi wa sehemu za Sumbawanga – Kanazi – Kizi – Kibaoni (km 151.6), Sitalike – Mpanda – Ifukutwa – Vikonge (km 73.65) umekamilika. Aidha, Mkataba wa ujenzi wa sehemu ya Vikonge – Luhafwe (km 25) umesainiwa na taratibu za kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa sehemu ya Luhafwe – Bulamata (km 37.35) zinaendelea.
Hadi kufikia Aprili 2022,Mkataba wa ujenzi wa sehemu ya Kibaoni – Sitalike (km 71.0): sehemu ya Kibaoni – Mlele (km 50) umesainiwa tayari kwa kuanza ujenzi. Aidha, taratibu za manunuzi kwa ajili ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa sehemu ya Sitalike – Mlele (km 21) zinaendelea. Vile vile,Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa sehemu ya Kizi – Lyambalyamfipa – Sitalike (km 86.31).
84.Mheshimiwa Spika, katika Barabara ya Nyanguge – Musoma, Mchepuo wa Usagara – Kisesa na Bulamba – Kisorya (km 202.25) ujenzi wa sehemu ya Usagara – Kisesa (Mwanza Bypass, km 16.35) na ukarabati wa sehemu ya Simiyu/Mara Border – Musoma (km 85.5) umekamilika. Aidha,Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ukarabati wa Barabara ya Nyanguge – Simiyu/Mara Border (km 100.4).
85.Mheshimiwa Spika, kuhusu Barabara ya Magole – Mziha – Handeni (km 149.2), mradi umekamilika kwa sehemu ya Magole – Turiani (km 48.8). Aidha, hadi kufikia Aprili, 2022 maandalizi ya ujenzi wa sehemu ya Turiani – Mziha – Handeni (km 104) yalikuwa yanaendelea.
86.Mheshimiwa Spika, mradi wa Ujenzi wa Barabara za Juu (Flyovers) Jijini DSM na Barabara Unganishi umeendelea kutekelezwa ambapo kazi zilizokamilika ni ujenzi wa Mfugale Flyover na "Interchange" ya Ubungo (Kijazi Interchange). Aidha, kazi za upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa mradi wa Ujenzi wa Barabara za Juu (Flyovers) kwenye Makutano Nane (8) ya Barabara za Jijini Dar es Salaam (Mwenge, Morocco, Magomeni, Selander, Fire, Osterbay, Buguruni na Tabata) zimekamilika. Vilevile, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa Ujenzi wa Mabey Flyovers Jijini Dar es Salaam, Dodoma na Mwanza.
87.Mheshimiwa Spika,kuhusu Barabara ya Mwigumbi – Maswa – Bariadi – Lamadi (km 181.8), mradi umekamilika kwa sehemu za Bariadi – Lamadi (km 71.8), Mwigumbi – Maswa (km 50.3) na Maswa – Bariadi (km 49.7). Aidha, ujenzi wa barabara ya Mchepuo wa Maswa (km 11) unaendelea na umefikia asilimia 10. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha za ujenzi wa sehemu ya Isabdula (Magu) – Bukwimba Station – Ngudu – Ng'hungumalwa (km 53).
88. Mheshimiwa Spika,hadi kufikia Aprili 2022, maandalizi ya ujenzi wa Barabara ya Tabora – Ipole – Rungwa (Sehemu ya Ipole – Rungwa, km 172) yalikuwa yanaendelea.Aidha, katika Barabara ya Kidahwe – Kasulu – Kibondo – Nyakanazi (km 341.25), ujenzi wa sehemuya Kidahwe – Kasulu (km 63.0) na Nyakanazi – Kakonko (Kabingo) (km 50) umekamilika. Aidha, ujenzi wa sehemu ya Kanyani Junction – Mvugwe (km 70.5) umefikia asilimia 17.14, Mvugwe – Nduta Junction (km 59.35) umefikia asilimia 25, Kibondo Junction – Kabingo (km 62.5) umefikia asilimia 20 na Nduta Junction – Kibondo (km 25.9) umefikia asilimia 44.1. Vilevile, taratibuza manunuzi ya Mkandarasi wa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Kibondo – Mabamba (km 48) zinaendelea.
89.Mheshimiwa Spika, kazi za ujenzi wa Barabara ya Kwenda Kiwanja cha Ndege cha Mafia (km 16) zimekamilika. Kuhusu mradi wa ujenzi wa Daraja la Nyerere (Kigamboni) na Barabara Unganishi, ujenzi wa Daraja la Nyerere, barabara ya Kigamboni (Daraja la Nyerere) – Vijibweni (km 1.5)na barabara ya Tungi – Kibada (km 3.8) umekamilika.Aidha, taratibu za manunuzi kwa ajili ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara ya Kibada – Mwasonga – Tundwisongani Jct/Tundwisongani – Kimbiji (km 41.0) zinaendelea.
90.Mheshimiwa Spika, taratibu za manunuzi kwa ajili ya kumpata Mhandisi Mshauri wa kufanya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina kwa ajili ya ukarabati kwa kiwango cha lami wa barabara ya Mutukula – Bukoba – Muhutwe – Kagoma (km 112) zinaendelea. Aidha, kazi za upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Bukoba – Busimbe – Maluku – Kanyangereko – Ngongo (km 19.1) na Kanazi (Kyetema) – Ibwera – Katoro – Kyaka II (km 60.7)zinaendelea.
91.Mheshimiwa Spika, kuhusu mradi wa upanuzi wa Barabara ya Kimara – Kibaha (km 19.2) ikijumuisha Upanuzi wa Madaraja ya Kibamba, Kiluvya na Mpiji, ujenzi wa barabara hii unaendelea. Hadi Aprili, 2022 mradi umefikia asilimia 86 baada ya nyongeza ya kazi za mkataba. Aidha, Serikali inaendelea kutafuta fedha za ujenzi wa Barabara ya Kisarawe – Mlandizi (km 119) kwa kiwango cha lami.
92.Mheshimiwa Spika, kuhusu mradi wa ujenzi wa Barabara ya Pugu – Kifuru – Mbezi Mwisho – Mpiji Magoe – Bunju (km 34.0), hadi kufikia Aprili, 2022 kazi za upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabaraza Mbezi Mwisho – Mpiji Magoe – Bunju (km 21.3) na Pugu – Kifuru – Mbezi Mwisho (km 12.7)kwa ajili ya kuijenga kwa njia sita ilikuwa katika hatua ya manunuzi.Serikali inaendelea kutafuta fedha za kazi hizi.
93.Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabara ya Muleba – Kanyambogo – Rubya (Leopord Mujungi km 18.5) katika mradi wa Barabara ya Kagoma – Lusahunga (km 172.5) umekamilika.
94.Mheshimiwa Spika, mkataba wa kufanya Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa Barabara ya Singida – Shelui (km 110) umesainiwa. Kuhusu Barabara ya Dar es Salaam – Mbagala (Kilwa Road) – Gerezani (Sehemu ya Kamata – Bendera Tatu km 1.3) hadi Aprili, 2022 kazi za Upanuzi wa Daraja la Gerezani zilikuwa zimefikia asilimia 78.8. Utekelezaji wa mradi ulisimama kutokana na changamoto za UVIKO 19. Aidha, Serikali inaendelea kutafuta fedha za upanuzi na ukarabati wa sehemu ya Mbagala Rangi Tatu – Kongowe (km 3.8).
95.Mheshimiwa Spika, katika Barabara ya Msimba – Ruaha Mbuyuni/Ikokoto Mafinga (km 535.25) kazi za ukarabati kwa sehemu ya Mafinga – Igawa (km 137.9) na usanifu wa kina wa sehemu ya Mafinga – Mgololo (km 78) umekamilika. Aidha, hadi kufikia Aprili, 2022, maandalizi ya ujenzi wa sehemu ya Rujewa – Madibira – Mafinga (km 152.0) yanaendelea. Kuhusu barabara yaMorogoro – Iringa (Tumbaku Jct. Mangae/Melela – Mikumi – Iyovi) (km 158.45), taratibu za manunuzi kwa ajili ya kumpata Mhandisi Mshauri wa kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ukarabati wa barabara hiyo zinaendelea.
96.Mheshimiwa Spika, katika Barabara ya Same – Mkumbara – Korogwe (km 147.5), upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa sehemu za Same – Himo (km 76.0) na Mombo – Lushoto (km 32) umekamilika na Serikali inaendelea kutafuta fedha za ukarabati kwa kiwango cha lami wa barabara hizi. Aidha, Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya upembuzi na usanifu wa kina wa barabara ya Lushoto – Magamba – Mlola (km 34.5).
Kwa upande wa barabara ya Same – Kisiwani – Mkomazi (km 97); upembuzi yakinifu na usanifu wa kina umekamilika. Mkandarasi kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara hii kwa sehemu yenye urefu wa kilometa 5.2 amepatikana.
97.Mheshimiwa Spika, katika mradi wa Barabara ya Mbeya – Makongolosi (km 267.9), kazi za ujenzi zimekamilika kwa sehemu za Mbeya – Lwanjilo – Chunya (km 72) na Chunya – Makongolosi (km 39).Mkataba wa ujenzi wa sehemu ya Noranga – Itigi – Mkiwa (km 56.9) umesainiwa. Aidha, Serikali inaendelea kutafuta fedha za ujenzi wa barabara ya Makongolosi – Rungwa – Noranga (km 356) na Mbalizi – Makongolosi (km 50) kwa kiwango cha lami.
98.Mheshimiwa Spika, katika Barabara ya Itoni – Ludewa – Manda (km 211), kazi za ujenzi kwa kiwango cha zege kwa sehemu yaLusitu – Mawengi (km 50) zinaendelea na zimefikia asilimia 85. Aidha, hadi kufikia Aprili 2022, mkataba wa ujenzi wa sehemu ya barabara ya Itoni – Lusitu (km 50) umesainiwa.
99.Mheshimiwa Spika, katika mradi wa Handeni – Kibirashi – Kijungu – Kibaya – Njoro – Olboloti – Mrijo Chini – Dalai – Bicha – Chambalo – Chemba – Kwa Mtoro – Singida (km 460), mkataba wa ujenzi wa sehemu ya Handeni – Mafuleta (km 20) umesainiwa na sehemu ya Mafuleta – Kibirashi (km 30) zipo katika hatua za manunuzi ya Mkandarasi wa ujenzi. Aidha, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara yaKongwa – Kibaya – Arusha (km 430)na Singida – Sepuka – Ndago – Kizaga (km 75) umekamilika.
100.Mheshimiwa Spika, kuhusu Barabara ya Makambako – Songea na Barabara ya Mzunguko ya Songea (km 295), hadi kufikia Aprili 2022, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwenye barabara ya mchepuo ya Songea umekamilika.Aidha,taratibu za kupata fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya kugharamia ukarabati wa barabara ya Makambako – Songea (km 295) zinaendelea.
101.Mheshimiwa Spika, kuhusu ujenzi wa Barabara ya Dodoma – Iringa (km 273.3), hadi kufikia Aprili 2022, ujenzi kwa kiwango cha lami wa mita 450 za Barabara ya Mchepuo wa Iringa (km 7.3) ulikuwa umekamilika na ujenzi wa madaraja madogo kwenye sehemu iliyobaki unaendelea. Aidha, kazi za uimarishaji wa matabaka ya barabara katika barabara yaIringa – Dodoma (km 266) zinaendelea.
102.Mheshimiwa Spika, mradi wa ujenzi wa Barabara ya Dodoma – Babati (km 263.4) umekamilika kwa sehemu ya Dodoma – Mayamaya – Mela – Bonga – Babati (km 250.8). Aidha, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Mchepuo wa Babati (km 15.5) umekamilika.
103.Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabaraya Masasi – Songea – Mbamba Bay (km 623) umekamilika. Kuhususehemu ya Kitai – Lituhi (km 90), ujenzikwa kiwango cha lami wa kilometa 5 umekamilika na mkataba wa ujenzi wa sehemu ya Amanimakoro – Ruanda (km 35) umesainiwa tarehe 14 Aprili, 2022. Aidha, taratibu za manunuzi kwa ajili ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa sehemu iliyobakia kilometa 50 za barabara hii zinaendelea.
104.Mheshimiwa Spika, kuhusu mradi wa Barabara za Chuo cha Uongozi (Uongozi Institute, km 8.8) Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami.
105.Mheshimiwa Spika, kuhusu Barabara za Igawa – Songwe – Tunduma na Mchepuo wa Mbeya (km 273.40), hadi kufikia Aprili 2022, upembuzi yakinifu na usanifu wa kinawa barabara ya Igawa – Songwe – Tunduma (km 218.0)na Uyole – Songwe (Mbeya Bypass, km 48.9) umekamilika. Taratibu za manunuzi kwa ajili ya kumpata Mkandarasi wa ukarabati wa sehemu ya Uyole – Ifisi (km 29) zinaendelea. Aidha, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Iwambi – Mbalizi Bypass (km 6.5) ziko katika hatua za manunuzi.
106.Mheshimiwa Spika, kuhusumradi wa Miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Pili Hadi Tano (BRT Phase II – V: km 69.8), kazi za ujenzi wa barabara ya Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Pili (CBD – Mbagala, km 20.3) zimefikia asilimia 50. Aidha, mkataba wa ujenzi wa miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Tatu (CBD – Gongolamboto km 23.33) umesainiwa. Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Nne (Ali Hassan Mwinyi – Morocco - Mwenge – Tegetana Mwenge – Ubungo km 30.12). Kuhusu mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Tano unaohusisha ujenzi wa barabara ya Bandari ya Dar es Salaam - Mandela – Kawawa – Kigogo – Tabata – Segerea (km 26.5), kazi ya upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina umekamilika.
Kuhusu Maboresho ya Barabara za BRT Awamu ya Kwanza (Jangwani), hadi kufikia Aprili, 2022, kazi ya usanifu wa kina zimekamilika katika eneo la Jangwani chini ya Mradi wa Maboresho ya Usafiri Dar es Salaam (DUTP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.
107.Mheshimiwa Spika,kuhusu mradi wa Ujenzi wa Jengo la Makao Makuu ya Taasisi ya Teknolojia ya Ujenzi (Institute of Construction Technology – ICoT), hadi Aprili, 2022, ujenzi wa jengo jipya la Taaluma na Utawala ICoT Morogoro upo katika hatua ya kumpata Mkandarasi. Aidha, Ujenzi wa Makao Makuu ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), unaendelea na mradi umefikia asilimia 40.5.
108.Mheshimiwa Spika, fedha za Mfuko wa Barabara zinatumika kutekeleza miradi mbalimbali ya barabara nchini. Kazi zilizopangwa kutekelezwa kwa mwaka 2021/22 katika Barabara Kuu kwa kutumia fedha za Mfuko wa Bar