Kazi za Kitengo cha Ukaguzi

Kufanya kazi kwa uhuru na kuhakikisha kunakuwa na mashauriano juu ya kazi ambazo zimeundwa kwa ajili ya kuongeza thamani na kuboresha kazi za Wakala.

Kitengo hiki kitafanya shughuli zifuatazo:

(i) Kusimamia na kuratibu shughuli zote za ukaguzi wa ndani wa Wakala kulingana na utaratibu na miongozo iliyowekwa.

(ii) kukagua na kutekeleza mpango wa ukaguzi wa ndani wa mwaka na mpango mkakati wa ukaguzi wa ndani.

(iii) Kukagua, kuangalia na kuthamini utoshelevu na utumiaji wa uhasibu, udhibiti wa kifedha na shughuli zingine za uendeshaji na kukuza udhibiti madhubuti kwa gharama nafuu.

(iv) Kushauri juu ya udhibiti wa ndani, usimamizi sahihi wa mali na kiwango sahihi cha kufuata juu ya kanuni, sera, mipango, taratibu na maagizo mengine ya Wakala.

(v) Kutoa uhakikisho kuwa Wakala unafuata sera, mipango na taratibu zilizowekwa.

(vi) Kutoa uhakikisho wa kuwa mali za Wakala zinahesabiwa na zinalindwa na upotevu wa aina yoyote.

(vii) Kutoa uhakikisho kwamba michakato ya usimamizi wa dharura au vihatarishi inafanya kazi vizuri na kwamba dharura na vihatarishi vinasimamiwa kwa kiwango kinachokubalika.

(viii) Kutathmini utendaji bora wa kazi katika kutekeleza majukumu iliyokasimishwa.

(ix) Kutoa mapendekezo ya namna ya kuboresho udhibiti wa ndani na michakato ya kusimamia vihatarishi/ dharura.

(x) Kuunda mahusiano mazuri na ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Wakaguzi wa nje) na ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani na wakaguzi wengine kutoka nje ya wakala.

(xi) Kuhakiki, kufuatilia, kutathmini na kupendekeza juu ya mifumo bora ya ukusanyaji mapato ya Wakala kwa ajili ya uwajibikaji sahihi.