Sehemu ya Ufundi na Ukodishaji Mitambo

Sehemu hii itafanya shughuli zifuatazo:

(i) Kuratibu uundaji wa mipango ya muda mfupi na muda mrefu ya kazi za ufundi.

(ii) Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa kazi na mipango kuhusu ufundi.

(iii) Kuanzisha na kukuza sera, na mipango itakayochochea huduma bora za ufundi na matengenezo.

(iv)Kuangalia utekelezaji wa huduma za ufundi na shughuli za matengenezo katika vituo vya uzalishaji .

(v) Kumsaidia mkurugenzi juu ya kukuza na kuhuisha vifaa vya uzalishaji na matengenezo, miongozo na viwango juu ya masuala ya ufundi.

(vi) Kuunda na kuanzisha utekelezaji wa viwango vya ubora wa matengenezo kwa kazi za ufundi.

(vii) Kuratibu na kunganisha ripoti za kazi za ufundi na kuziwasilisha kwa mkurugenzi wa uzalishaji, matengenezo na ukodishaji mitambo kwa ujumuishaji.

(viii) Kuratibu uundaji wa mipango ya huduma ya ukodishaji mitambo ya muda mfupi na muda mrefu.

(ix) Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa mipango ya huduma ya ukodishaji mitambo.

(x) Kuanzisha na kukuza sera, programu na mipango itakayochochea huduma bora za ukodishaji mitambo.

(xi) Kuunda na kuanzisha mipango madhubuti ya utekelezaji wa viwango vya matengenezo vya ubora wa ukodishaji mitambo.

(xi) Kuratibu na kujumuisha ripoti za ukodishaji mitambo mara kwa mara.

.