Sehemu ya Rasilimali Watu na Utawala
Sehemu hii itafanya shughuli zifuatazo:
(i) Kutafsiri sera na miongozo ya rasilimali watu kwa Wakala na watumishi kwa lengo la kufuata viwango sahihi na kupunguza migogoro au kupotoka kwa utendaji bora.
(ii) Kufuatilia, kuhakiki rekodi zote za rasilimali watu pamoja na pensheni, upandaji wa madaraja, uhamisho, na ukomo wa ajira kwa kutumia data zilizohuishwa kwa ajili ya kupanga na kufanya maamuzi.
(iii) Kusimamia mchakato wa ajira na kuajiri watumishi wapya kulingana na mahitaji ya idara husika kwa ajili ya kujaza nafasi za wazi ili kufikia malengo ya Wakala.
(iv) Kuendeleza na kudumisha mipango ya mafunzo pamoja na mwelekeo wa watumishi, mafunzo ya muda mfupi na mafunzo ya muda mrefu ili kukuza mitizamo bora ya utendaji wa Wakala.
(v) Kusimamia malalamiko ya watumishi ili kudumisha uhusiano bora wa kazi baina ya watumishi na kutatua kero zao kwa lengo la kudumisha maelewano katika Wakala.
(vi) Kuhuisha mfumo wa malipo ya watumishi wa Wakala kulingana taratibu na miongozo iliyowekwa.
(vii) Kufuatilia na kusimamia operesheni ya Mfumo wa (HCMIS) katika Wakala.
(viii) Kuratibu masuala ya ajira, uteuzi, kujaza nafasi zilizo wazi, uthibitisho kazini na uhamisho kwa watumishi wa Wakala.
(ix) Kuratibu mipango na maendeleo ya rasilimali watu.
(x) Kuratibu utekelezaji wa tathmini ya utendaji kazi kwa watumishi.
(xi) Kusimamia mafao ya wastaafu pamoja na watumishi ikiwa ni pamoja na pensheni, posho.
(xii) Kupangilia utunzaji sahihi wa sajili/rejesta kwa kuhakikisha kunakuwepo na fanicha bora kwa utunzaji salama wa nyaraka na kuweka alama sahihi kwa lengo la kulinda, kusimamia upatikanaji wa hati kwa urahisi kwa ajili ya matumizi ya ofisi.
(xiii) Kuratibu na kusimamia usafi wa majengo ya ofisi, utunzaji wa vifaa na mazingira ya ofisi kwa kutoa zana zinazofaa kutumika katika kufagia, kufuta, kusafisha sakafu na kuing'arisha, kutunza bustani nakusimamia utupaji sahihi wa takataka ili kudumisha usafi wa majengo ya ofisi, vifaa na mazingira ya karibu.