Kitengo cha Masoko na Uhusiano

Kitengo hiki kinawajibika kwa kuanzisha na kudumisha uhusiano bora baina ya Wakala na umma.


Kitengo kitafanya shughuli zifuatazo;

(i) Kuendeleza na kutekeleza mipango mkakati ya uhusiano kwa umma ili kufikia ongezeko kubwa katika uhamasishaji na kuhakikisha umma unafahamu kuhusu huduma zinazotolewa na Wakala.

(ii) Kuanzisha malengo ya uhusiano kwa umma ya Wakala.

(iii) Kushauri juu ya maendeleo, muundo, utekelezaji na tathmini ya taarifa mbalimbali, mipango, miradi na huduma zingine za Wakala.

(iv) Kufanya tafiti za masoko, kukuza na kutekeleza mipango ya masoko.

(v) Kutangaza huduma za TEMESA kwa umma.

(vi) Kufanya tafiti za masoko na jinsi ya kukuza soko ili kuongeza tija kwenye maswala ya masoko.

(vii) Kuratibu shughuli zote za uhusiano kwa umma

(viii) Kusimamia maswali ya habari na maombi ya mahojiano.

(ix) Kuendeleza na kukagua aina ya mipango ya uendelezaji, mpango mkakati wa kutangaza huduma na utoaji wa taarifa mbalimbali pamoja na namna ya kuelekeza taarifa hizo katika vyombo husika.

(x) Kusimamia mawasiliano wakati wa majanga na kuanzisha itifaki sahihi ya kufuata ya kimawasiliano inapotokea majanga kwa Wakala.

(xi) Kusimamia na kupakia habari kwenye wavuti ya Wakala na mitandao ya kijamii.