Sehemu ya Ujenzi na Matengenezo ya Vivuko

Sehemu hii itafanya shughuli zifuatazo:

(i) Kubuni mipango na mikakati ya kuboresha huduma za vivuko.

(ii) Kuandaa mpango kazi wa muda mrefu na wa muda mfupi kwa ajili ya programu za ujenzi na matengenezo ya maegesho ya vivuko.

(iii) Kuorodhesha mahitaji ya ujenzi wa vivuko vipya na ujenzi wa maegesho mapya.

(iv) Kuandaa bajeti ya ujenzi na matengenezo vivuko ya mwaka, robo mwaka, nusu mwaka na ripoti za mwaka mzima.

(v) Kuchambua, kusimamia, kufuatilia na kukagua utendaji wa kila siku wa vivuko.

(vi) Kuanzisha ratiba za matengenezo kinga ya mara kwa mara ya vivuko katika vituo vyote.

(vii) Kuanzisha taratibu na kanuni za usafi, matengenezo na usimamizi wa zana za usafi katika vivuko vyote.

(viii)Kuhakikisha taarifa zote zinazohusiana na masuala ya ujenzi na matengenezo ya vivuko zinakusanywa kwa wakati.