Sehemu ya Uendeshaji na Usalama wa Vivuko

Sehemu hii itafanya shughuli zifuatazo:

(i) Kuandaa mpango kazi wa muda mrefu na muda mfupi kwa ajili ya programu za uendeshaji na usalama wa vivuko.

(ii) Kuanzisha na kusimamia utekelezaji wa viwango na taratibu za usalama wa kivuko.

(iii) Kusimamia na kushirikiana kwa pamoja na mameneja wa mikoa juu ya njia bora zaidi za kuboresha utendaji kazi wa vivuko na usalama wa vivuko.

(iv) Kufuatilia na kusimamia ukusanyaji wa mapato ya kila siku katika vituo vyote vya vivuko nchini.

(v) Kutathmini hali ya vifaa vya uokozi na usalama watumishi wa vivuko wanapokuwa ndani ya kivuko ili kuhakikisha kuwa wote wanatimiza mahitaji ya usalama wakati wote.

(vi) Kutathmini ufanisi wa huduma za vivuko na taratibu za usalama na kuushauri Wakala kupitia mkurugenzi.

(vii) Kupanga na kuratibu mafunzo kwa watumishi wa vivuko kuhusu masuala yanayohusu usalama wa vivuko.

(viii) Kuhakikisha taarifa zote zinazohusiana na masuala ya uendeshaji na usalama wa vivuko zinakusanywa kwa wakati.