Tunafanya nini?
Majukumu ya msingi ya Wakala ni kama ifuatavyo:
(i) Kufanya matengenezo ya Magari, pikipiki na Mitambo ya Serikali katika Karakana ambazo zipo kila Mkoa;
(ii) Kufanya matengenezo na Usimikaji wa Mifumo ya Umeme, Mabarafu, viyoyozi na Elektroniki;
(iii) Kufanya matengenezo ya taa za kuongozea magari (Traffic Signals) na taa za barabarani (Street Lights);
(iv) Kukodisha magari kwa ajili ya usafiri wa Viongozi (VIP Vehicles) yaliyopo katika Kitengo cha GTA (Government Transport Agency) ;
(v) Kukodisha mitambo ya kuzalisha kokoto, na mitambo ya kazi za barabara;
(vi) Uendeshaji wa Vivuko vya Serikali;
(vii) Kutoa ushauri wa Kitaalamu kwa Serikali na Umma kwa ujumla katika nyanja za uhandisi wa Ufundi, Umeme na Elektroniki;
(viii) utoa ushauri wa kitaalamu kuhusu usimikaji wa mifumo mipya ya uhandisi wa Ufundi, Umeme na Elektroniki; na
(ix) Kufanya usanifu na Usimamizi wa usimikaji wa mifumo ya uhandisi wa Ufundi Umeme na Elektroniki ili kukidhi viwango vinavyotakiwa na kwa kulingana na matakwa ya Sheria na Taratibu zinazoongoza taaluma husika.