Sehemu ya Umeme na Elektroniki

Sehemu hii itafanya shughuli zifuatazo:

(i) Kuratibu na kuunda programu za muda mfupi na za muda mrefu za umeme na elektroniki.

(ii) Kuratibu na kusimamia utekelezaji wa kazi za umeme na elektroniki.

(iii) Kuanzisha na kukuza sera, mipango na programu ambazo zitaongeza na kuchochea ubora wa bidhaa za umeme na elektroniki na kazi za matengenezo.

(iv) Kufuatilia utekelezaji wa shughuli za kazi za umeme na elektroniki katika vituo vya uzalishaji.

(v) Kuendeleza na kuhuisha kazi za matengenezo na huduma za ufundi, miongozo na viwango juu ya maswala ya umeme na elektroniki.

(vi) kuunda na kuanzisha utekelezaji wa viwango vya ubora wa matengenezo ya kazi za umeme na elektroniki.

(vii) Kuratibu na kuunganisha ripoti za shughuli za umeme na elektroniki.