Mkurugenzi wa Idara ya Huduma Saidizi
Mkurugenzi atafanya kazi zifuatazo;
(i) Kusimamia mipango na masuala ya bajeti katika Wakala.
(ii) Kutengeneza mipango mbalimbali ya Wakala na kuhakikisha utekelezaji wake na ukaguzi wa mara kwa mara.
(iii) Kukamilisha mahitaji ya rasilimali watu ili kufikia malengo ya Wakala.
(iv) Kuhakikisha muundo na michakato inaunga mkono dhima, malengo na shughuli za Wakala.
(v) Kuongeza juhudi katika mambo ambayo yanaongeza thamani katika uzalishaji, matengenezo, huduma za vivuko, ushauri, huduma za kukodisha mitambo na shughuli za ubunifu kwa Wakala.
(vi) Kupanga, kuelekeza na kudhibiti shughuli za uhasibu wa kifedha wa Wakala.
(vii) Kupanga, kukuza, kukagua vyombo vya kufanya kazi vya Wakala ikiwa ni pamoja na kufuata muongozo wa utoaji wa huduma, kanuni za watumishi, motisha kwa watumishi, mpango wa urithishaji wa madaraka;
(viii) Kuhakikisha usimamizi mzuri wa rasilimali watu na mafunzo kwa watumishi.
(ix) Kusimamia, kuelekeza na kutoa ushauri juu ya mambo yote yanayohusu fedha, uhasibu na upangaji pamoja na fedha na mali zingine za Wakala.