Sehemu ya Fedha na Uhasibu
Sehemu hii itafanya shughuli zifuatazo:
(i) Kuandaa taarifa za kifedha za akaunti za mwaka mzima.
(ii) Kutoa idhini ya malipo, kusaini na kutoa hundi za malipo.
(iii) Kusimamia akaunti ya benki inayoendeshwa na afisa uhasibu.
(iv) Kuandaa ripoti za kifedha za mwaka kama ilivyo kwenye muongozo wa uhasibu wa Wakala na Sheria ya Fedha za Umma..
(v) Kusimamia usalama wa nyaraka za uhasibu, utunzaji wa vocha na usajili kamili wa bachi.
(vi) Kusimamia masuala ya ukaguzi na majibu ya maswali juu ya ripoti za uchunguzi / ukaguzi.
(vii) Kusimamia mwenendo wa kifedha wa Wakala ili kuhakikisha kuwa kuna fedha za kutosha kukidhi majukumu ya sasa ya Wakala.
(viii) Kutunza na kuhuisha kumbukumbu za madeni.
(ix) Kuandaa ripoti za kifedha na kuchambua na kukagua ripoti za utendaji wa kila mwezi