MPANGO MKAKATI

Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) imeandaa mpango mkakati wa miaka mitano kuanzia 2016/17 hadi 2020/21 ili kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia malengo makuu saba (7) ya kimkakati. Malengo hayo yanaenda sambamba na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) 2015 na matarajio ya wadau na sera mbalimbali za kitaifa.

Malengo hayo ya kimkakati ya wakala ni:

(i) Maambukizi ya VVU/UKIMWI yanapungua na huduma saidizi zinaboreshwa;

(ii) Utekelezaji wa mpango wa Taifa wa kupambana na rushwa unaimarishwa;

(iii) Mifumo ya kifedha inaboreshwa na kuwa endelevu;

(iv) Huduma za kihandisi na miundombinu husika inaboreshwa;

(v) Huduma na mifumo ya utendaji inaboreshwa;

(vi) Utawala bora na uwajibikaji unaimarishwa;

(vii) Usimamizi wa rasilimali watu unaboreshwa.