Sehemu ya Mipango na Usimamizi

Sehemu hii itafanya shughuli zifuatazo:

(i)Kutoa mwongozo wa kiufundi na msaada kitaasisi kuhusu mipango mkakati na mchakato wa bajeti.

(ii) Kuratibu uundaji na utayarishaji wa mipango ya mwaka, mipango ya biashara na mipango mkakati ya kati.

(iii) Kushiriki katika kuchambua kazi wa utaftaji wa kazi zisizo za msingi (Ushiriki wa Sekta Binafsi)

(iv) Kufuatilia utekelezaji wa mipango ya kila mwaka, mipango ya biashara na mipango ya mikakati ya kati.

(v) Kuandaa ripoti za utendaji wa kila wakati ikiwa ni pamoja na ripoti za robo, katikati na mwaka.

(vi) Kukusanya, kupitia na kuchambua takwimu zinazohitajika katika uundaji na utekelezaji wa mipango na mapendekezo ya bajeti.

(vii) Kushiriki katika kuandaa mipango, programu na shughuli za bajeti za Wakala na uundaji wa malengo na viashiria vya utendaji.

(viii) Kufanya tafiti na kuangalia athari za tafiti za mipango, miradi na programu zilizofanywa na Wakala.

(ix) Kufanya uchambuzi wa soko ili kutafuta fursa na kutambua mahitaji ya wateja na kuboresha huduma kwa wateja.

(x)Kuendelea kukuza na kutangaza huduma za TEMESA.

(xi) Kufanya tafiti za wateja kama vile huduma bora kwa wateja, kuandaa na kuwasilisha ripoti kwa ajili ya matumizi ya menejimenti.