TEMESA YAWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI KWA KAMATI YA BUNGE YA KUDUMU YA UWEKEZAJI NA MITAJI YA UMMA
Posted On: August 05, 2026
Uongozi wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri Bw. Andrew W. Massawe, chini ya uongozi wa Wizara ya Ujenzi ulioongozwa na Naibu Katibu Mkuu Bw. Charles Msonde, leo tarehe 5 Agosti, 2026 umewasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wakala mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma.
Wakati wa uwasilishaji wa taarifa hiyo, Mtendaji Mkuu Bw. Kheri Mahimbali amewasilisha taarifa mbalimbali kuhusu utekelezaji wa majukumu, ukusanyaji wa mapato, maendeleo ya miradi pamoja na hatua zinazochukuliwa kuendelea kuboresha utoaji wa huduma ziliwasilishwa kwa Kamati kwa ajili ya kujadiliwa na kupokea maelekezo ya kuimarisha utendaji wa Wakala.
TEMESA inaendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi katika kuhakikisha huduma za uhandisi, matengenezo ya magari na mitambo, pamoja na usimamizi na uendeshaji wa vivuko zinatolewa kwa viwango vinavyokidhi matarajio ya Serikali na wananchi.