BODI YA USHAURI YAPONGEZA MABORESHO YA MUUNDO TEMESA
Posted On: August 10, 2026
Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) imeipongeza Menejimenti ya Wakala kwa hatua mbalimbali za maboresho yanayoendelea, yakiwemo maboresho ya muundo wa Wakala, yanayolenga kuimarisha ufanisi, uwajibikaji na kasi ya utoaji huduma kwa wananchi.
Pongezi hizo zimetolewa Agosti 7 2026, wakati wa kikao kazi cha Bodi ya Ushauri kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Cate Mkoani Morogoro.
Akizungumza wakati wa kikao hicho,wenyekiti wa Bodi hiyo Bw. Andrew Massawe, amesema Bodi imeridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Menejimenti katika kuimarisha utendaji wa TEMESA na kuhakikisha huduma zinazotolewa zinaendelea kuwa bora, zenye ufanisi na zinazokidhi mahitaji ya wananchi.
“Tunapongeza jitihada za Menejimenti katika kuendelea kufanya maboresho. Muundo huu ni hatua muhimu katika kuimarisha utendaji, uwajibikaji na ufanisi wa Wakala,” amesema Massawe.
Aidha, Bodi imeitaka Menejimenti kuendelea kusimamia utekelezaji wa maboresho hayo kwa ushirikiano, weledi na uwajibikaji, huku kila mtumishi akitekeleza majukumu yake kwa wakati na kuzingatia viwango vya kitaalamu.