TEMESA YASHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
Posted On: March 08, 2023
Leo tarehe 8 Machi, 2023, Wanawake Watumishi wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) kote nchini wameungana na wanawake wengine kote Duniani katika Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Wanawake Duniani. Katika Mkoa wa Dodoma, maadhimimisho hayo yamefanyika katika Viwanja vya Sabasaba Wilayani Kondoa Mkoani Dodoma, yakiwa na *Kaulimbiu
"UBUNIFU NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA CHACHU KATIKA KULETA USAWA WA KIJINSIA."