ULEGA APOKEA TAARIFA YA KAMATI UCHUNGUZI MV. TANGA

News Image

Posted On: May 22, 2025

Waziri wa Ujenzi, Mhe. Abdallah Ulega amepokea Taarifa ya Kamati ya uchunguzi ya Kivuko cha MV. TANGA kinachotoa huduma kati ya Pangani na Bweni Wilayani Pangani, Mkoani Tanga siku ya Mei 20, 2025 Ofisini kwake jijini Dodoma.

Kamati hiyo aliiunda Mei 13, 2025 alipofanya ziara mkoani Tanga na kuipa siku Saba kuchunguza changamoto zinazojitokeza mara kwa mara katika kivuko hicho baada ya kupokea malalamiko ya wananchi kuhusu kusuasua kwa utendaji wake.