UKARABATI KIVUKO CHA MV. PANGANI II WAKAMILIKA

News Image

Posted On: February 09, 2020

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Eng. Japhet Y. Maselle amekagua kivuko cha MV. PANGANI II baada ya Kukamilika kwa ukarabati wake. Kivuko hicho kimefanyiwa ukarabati mkubwa ikiwemo kubadilishiwa mfumo mpya na kuweza kufanya kazi kwenye maji ya bahari (maji chumvi) tofauti na hapo awali ambapo kilikuwa kikifanya kazi kwenye maji ya Mto (maji baridi), awali kilijulikana kama MV. UTETE na kilikuwa kikitoa huduma kati ya Utete na Mkongo Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani, kilishindwa kuendelea kutoa huduma maeneo hayo kutokana na changamoto ya kupungua kwa kina cha maji kwa muda mrefu katika Mto Rufiji. Kivuko hicho kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari 6 sawa na tani 50.