UKARABATI KIVUKO CHA MV. CHATO WAKAMILIKA

News Image

Posted On: November 05, 2018

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle leo amekagua kivuko cha MV. Chato ambacho ukarabati wake umemalizika hivi karibuni, tukio hilo limefanyika katika yadi ya Songoro iliyopo katika eneo la Ilemela mjini Mwanza. Kivuko hicho cha tani 75 kina uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 6 na kinatoa huduma katika Wilaya ya Chato, maeneo ya Ikumba Itale, Izumacheli, Muharamba, Senga, Bukondo na Bwina Mkoani Geita. Mkurugenzi Huduma za Ufundi (Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano) Mhandisi Lazaro Vazuri pamoja na Meneja wa TEMESA mkoa wa Mwanza Mhandisi Hassan Karonda walishiriki pia katika tukio hilo.