MAFUNZO YA MFUMO WA USIMAMIZI WA KAZI ZA MATENGENEZO KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WA TEMESA
Posted On: March 04, 2025
Katika Ukumbi wa Mikutano wa TEMESA mkoani Dodoma, kumefanyika kikao cha mafunzo kuhusu Mfumo wa Usimamizi wa Kazi za Matengenezo (MUM) ambapo Mafunzo haya yamehusisha Mabalozi, Wagavi na Mafundi wa TEMESA.
Lengo kuu la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo wa kutumia mfumo Pamoja na kuboresha ufanisi wa shughuli za matengenezo ya magari, umeme na huduma mbalimbali zitolewazo na TEMESA. Mfumo huu wa MUM utahakikisha usimamizi bora, uwazi, na ufanisi katika utekelezaji wa kazi za matengenezo, huku ukilenga kuongeza tija na kupunguza gharama zisizo za lazima.
Katika mafunzo haya, washiriki wamepata maelezo ya kina kuhusu matumizi sahihi ya Mfumo wa Usimamizi wa Kazi za Matengenezo, mbinu bora za ufuatiliaji wa matengenezo, na jinsi mfumo huu unavyoweza kusaidia katika kuboresha huduma za TEMESA kwa wadau wake.