KIVUKO KIPYA BUGOROLA UKARA MBIONI KUKAMILIKA

News Image

Posted On: October 05, 2020

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle, Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ufundi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Lazaro Vazuri Pamoja na wakurugenzi kutoka Wakala huo leo wamekagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko kipya cha Bugorola Ukara MV. UKARA II ambacho kinakaribia kukamilika tayari kwa kuanza kutoa huduma.

Kivuko cha Bugorola-Ukara ambacho ujenzi wake unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.2 kina uwezo wa kubeba abiria 300 na magari 10 sawa na tani 100.