TEMESA YASHIRIKI MAONESHO YA WAKULIMA NANENANE SIMIYU

News Image

Posted On: August 03, 2019

Wakala wa Ufundi na Umeme nchini TEMESA unashiriki Maonesho ya Wakulima Nanenane Kitaifa mwaka 2019 ambayo yameanza rasmi huko mkoani Simiyu, maonesho hayo yaliyofunguliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan yanafanyika Kanda ya Ziwa Mashariki katika viwanja vya Nyakabindi Mjini Bariadi.

Maonesho ya Nanenane Kitaifa yanafanyika kwa mara ya pili sasa mkoani Simiyu tangu Kanda ya Ziwa ilipogawanywa katika kanda mbili yaani, Kanda ya Ziwa Mashariki(Simiyu, Mara na Shinyanga) na Kanda ya Ziwa Magharibi(Mwanza, Geita na Kagera) ambapo mwaka huu yanaadhimishwa chini ya kauli Mbiu:-“KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KATIKA UKUAJI WA UCHUMI WA NCHI”