TEMESA YASHIKA NAFASI YA PILI TAASISI ZA UMMA NANENANE SIMIYU
Posted On: August 08, 2019
Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA umeshinda Cheti cha Ushindi pamoja na Kikombe kwa kuwa mshindi wa pili katika kundi la Taasisi za Umma kwenye Maonesho ya 27 ya Wakulima Nanenane Kitaifa Kanda ya Ziwa Mashariki yaliyokuwa yakifanyika katika Viwanja vya Nyakabindi Bariadi Simiyu. Maonesho hayo yamefungwa rasmi leo na Mh. Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania