TEMESA YAFUNGA TAA KUZUNGUKA UKUTA WA MACHIMBO YA MERERANI
Posted On: April 29, 2019
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle pamoja na mameneja wa mikoa mitatu wamekagua kazi ya ufungaji wa taa katika ukuta uliozunguka machimbo ya madini ya Tanzanite eneo la Mererani, Wilayani Simanjiro mkoani Manyara. Mradi huo wa ufungaji wa miundombinu ya taa ni agizo la mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa wakati wa ziara yake katika mgodi huo ambapo aliagiza ujenzi wa ukuta huo na kusisitiza ufungwe taa pamoja na kamera za ulinzi kwa ajili ya kulinda usalama wa mgodi huo. usimikaji wa taa hizo umesimamiwa na meneja wa Wakala huo kutoka mikoa ya Kilimanjaro Mhandisi Ferdinand Mishamo, meneja wa Arusha Mhandisi Heriel Mteri, pamoja na Meneja wa mkoa wa Dodoma Mhandisi Liberatus Bikulamchi.