TEMESA YAENDELEA KUTUMIA MAONESHO YA SABASABA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA WADAU WAKE
Posted On: July 10, 2026
Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) umeendelea kutumia Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) kuimarisha ushirikiano na wadau wake kupitia ziara za viongozi na majadiliano yanayolenga kuboresha utoaji wa huduma.
Katika kuendeleza jitihada hizo, leo tarehe 10 Julai, 2026, Kaimu Mkurugenzi wa Rasilimaliwatu na Utawala kutoka TEMESA, Bw. Nelson Rwechungura, akiongozana na Meneja wa TEMESA Mkoa wa Manyara, Mhandisi Aurelia Ngopa, wametembelea banda la TEMESA na baadaye kufanya ziara katika mabanda ya wadau mbalimbali wanaopatiwa huduma na TEMESA.
Ziara hiyo ilitoa fursa ya kubadilishana uzoefu, kuakisi utawala bora huku ikisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kufanikisha maendeleo na ustawi wa taasisi na utoaji huduma Bora.