TEMESA KUFUNGA TAA ZA BARABARANI MKOA WA SINGIDA

News Image

Posted On: May 18, 2022

Wakala wa Ufundi na Umeme nchini TEMESA kupitia Kikosi chake cha Umeme, uko mbioni kuanza kusimika taa za barabarani pamoja na taa za kuongozea magari zinazotumia umeme jua katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida, Meneja wa Kikosi cha Umeme kinachosimamia mradi huo Mhandisi Pongeza Semakuwa, amesema kuwa kikosi chake kinatarajiwa kuanza kazi hiyo kuanzia mapema wiki ijayo ambapo ameongeza kuwa taa hizo zitasimikwa katika eneo la Kintinku barabara ya Dodoma Singida na eneo la Malendi barabara ya Singida Tabora.

Ameongeza kuwa taa za kuongozea magari ambazo pia zinatumia umeme jua zinatarajiwa kusimikwa baada ya kukamilika kusimikwa kwa taa za barabarani ambapo taa hizo zitasimikwa Katika makutano ya barabara ya Uhasibu. Kazi ya kuandaa vifaa vitakavyotumika kwa ajili ya kusimika taa za kuongozea magari tayari imeanza ambapo mafundi wa Kikosi hicho tayari wamekwisha anza kujenga vizuizi vya kulinda taa hizo pamoja na mashimo kwa ajili ya kuanza kusimika taa.

Mradi huo umegharimu jumla ya shilingi milioni 386,645,160.

Tanzania Census 2022