TEMESA KUSIMIKA MIFUMO YA UMEME JENGO JIPYA LA HALMASHAURI YA MJI BARIADI
Posted On: December 10, 2021
Ofisi ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mkoa wa Simiyu imesaini mkataba wa kusimika mifumo ya umeme na viashiria vya moto katika jengo jipya la halmashauri ya mji wa Bariadi, mkataba huo ambao gharama yake ni shilingi milioni 177.5, umesainiwa kati ya Meneja wa TEMESA Mkoa wa Simiyu Mhandisi Ramadhan M. Ally pamoja na Meneja wa Wakala wa Majengo Mkoa wa Simiyu Mhandisi Abubakar A. Shekhan , kazi ya usimikaji wa mifumo hiyo tayari imekwishaanza na inatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi April, 2022.