WATUMISHI TEMESA WAKUTANA KWA MAPUMZIKO MOROGORO
Posted On: May 27, 2025
Watumishi kutoka Makao Makuu ya Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) wamekutana kwenye mapumziko ya pamoja katika hoteli ya Cate iliyoko Mkoani Morogoro kwa lengo la kutafakari pamoja na kujenga mahusiano mema kati ya watumishi nia na madhumuni na ikiwa ni kujenga umoja pamoja na kufanyia kazi malengo yao kwa umoja.
Mapumziko hayo yaliambatana na Kikao kilichoongozwa na Mtendaji Mkuu ambacho kililenga kuimarisha utendaji kazi, ushirikiano na kuamsha ari ya utendaji kazi kwa watumishi.
Akifungua kikao hicho Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Lazaro Kilahala, amesisitiza kuwepo na ushirikiano baina ya watumishi wa kada zote ili kuchochea maendeleo ya Taasisi na kujenga misingi imara ya mafanikio.
Pamoja na mambo mengine, watumishi hao pia walipata fursa ya kupewa semina na mafunzo kutoka kwa wataalamu mbalimbali akiwemo Meneja Rasilimaliwatu na Utawala Stanley Mulibo.
Kilahala pia aliwashukuru wastaafu na watumishi waliohama kwa mchango wao mkubwa walioutoa katika kuijenga Taasisi na kusisitiza kuwa uadilifu na bidii yao kazini vimeacha alama isiyofutika.