TEMESA YASHIRIKI MAONESHO YA KIMATAIFA YA 45 YA BIASHARA SABASABA

News Image

Posted On: July 03, 2021

Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) unawakaribisha wananchi wote katika Maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa ya Sabasaba yanayofanyika katika uwanja wa Maonesho wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere Sabasaba jijini Dar Es Salaam.

Banda la TEMESA lipo ndani ya Tent la Jakaya Kikwete banda namba 57&58. Ukifika katika banda letu utapata elimu kuhusu matumizi sahihi ya taa za kuongozea vyombo ya moto barabarani , Elimu ya jinsi ya kutumia maboya ya kujiokoa pindi inapotokea ajali ya kuzama kwa kivuko au moto ndani ya kivuko, pia utapata elimu kuhusu namna ya kutambua vipuri feki na vipuri halisi kutoka kwa wataalamu wetu wa matengenezo ya magari pamoja na elimu kuhusu matengenezo na usimikaji wa mifumo ya Umeme, mabarafu, viyoyozi pamoja na Elektroniki, huduma za vivuko pamoja na mitambo ya kukodisha.

Kauli Mbiu ya Maonesho hayo ni, ‘’Uchumi wa Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu.’’