SIKU YA PILI YA KIKAO CHA UTENDAJI KAZI

News Image

Posted On: January 30, 2022

''Mipango sahihi, umakini katika utekelezaji wa mipango, nidhamu ya matumizi ya rasilimali za Wakala na uwajibikaji wa kila mmoja wetu katika nafasi yake ndio mwelekeo tunaokwenda nao sasa na namna pekee tutaweza kuinua mafanikio na taswira ya Wakala. Kila mmoja wetu aitambue, kuithamini na kuiishi dhamana hii kubwa tuliyopewa.

Tunahuisha miongozo ya utendaji (operations manulas) na utafuatilia kwa karibu utendaji wetu katika misingi hii na hatutasita kuchukua hatua ili kuhakikisha haturudi nyuma.''

Lazaro N. Kilahala, Mtendaji Mkuu TEMESA akizungumza na mameneja na wakuu wa vituo katika ukumbi wa mikutano VETA Dodoma siku ya pili ya kikao cha Utendaji kazi wa vituo vya uzalishaji vya Wakala ambapo kwa nusu mwaka, Wakala umezalisha shilingi Bilioni 39,899,248.115 sawa na asilimia 69 ya lengo.