BODI YA USHAURI TEMESA YASISSITIZA MABADILIKO YA KIUTENDAJI KATIKA UTOAJI HUDUMA

News Image

Posted On: June 01, 2026

Menejimenti ya Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) imekutana na kufanya kikao cha pamoja na Bodi ya Ushauri ya TEMESA katika Ukumbi wa Mikutano wa TEMESA Makao Makuu jijini Dodoma.

Katika kikao hicho, Menejimenti ya Wakala imewasilisha taarifa mbalimbali za hali ya Wakala katika majukumu yake ambapo Mwenyekiti wa Bodi Bw. Andrew Massawe, amesisitiza mabadiliko ya kiutendaji katika utoaji wa huduma yanayopelekea kuleta mabadiliko ya huduma bora.

Aidha, Bodi imeishauri TEMESA kuunda namna sahihi ya ukusanyaji wa mrejesho kutoka kwa wadau wake ili kuchochea maboresho katika huduma zake.