TEMESA KUSIMIKA TAA ZA BARABARANI KISIWANI ZANZIBAR

News Image

Posted On: August 27, 2018

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji Zanzibar Bw. Mustafa Aboud Jumbe na kaimu Meneja wa Kikosi cha Umeme kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Pongeza Semakuwa wametia saini mkataba wa mradi wa kusanifu, kujenga na kusimika taa za kuongozea magari barabarani zitakazotumia umeme jua na umeme wa kawaida, tukio hilo lililofanyika katika ofisi za Wizara hiyo zilizopo barabara ya Fumba Kisauni kisiwani Unguja lilishuhudiwa na Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu, Mwanasheria TEMESA Bi. Joyce Senkondo, Mkurugenzi wa Mipango wa Wizara hiyo Ndg. Hatibu M. Hatibu, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Ndg. Shomari Shomari pamoja na baadhi ya maafisa wa Wizara hiyo. Mradi huo unakua wa kwanza kufanywa na TEMESA katika visiwa hivyo na utatekelezwa katika makutano ya Muzamili, Mjini kati, Mtoni na Kwa Pweza mjini Unguja na Mtemani na PBZ Chake Visiwani Pemba.