WATUMISHI WAMPOKEA RASMI MTENDAJI MKUU TEMESA

News Image

Posted On: May 14, 2026

Watumishi wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) wamempokea rasmi Mtendaji Mkuu mpya wa TEMESA Bwana Kheri Mahimbali ambaye ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza mara baada ya kuwasili katika ofisi za Makao Makuu ya TEMESA tarehe 6 Mei, 2026, Bw. Mahimbali amewashukuru watumishi kwa mapokezi mazuri na ya heshima waliyompatia na kuwaahidi kushirikiana nao kwa karibu wakati wote katika kutekeleza majukumu ya taasisi kwa ufanisi pamoja na kuzingatia uboreshaji wa maslahi ya watumishi ili kuongeza tija na ari ya utendaji kazi.

Aidha, Bw. Mahimbali amemshukuru Mhe. Rais kwa uteuzi huo na kuahidi kutekeleza maagizo yote kwa weledi na ufanisi ili kuhakikisha anafikia matarajio ya maboresho ya TEMESA na utoaji Huduma Bora.