BODI YA USHAURI TEMESA YAPATA MAFUNZO YA UONGOZI MOROGORO
Posted On: July 28, 2026
Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) inaendelea kupatiwa mafunzo ya uongozi yanayofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Cate Hotel, Mkoani Morogoro. Mafunzo hayo ya siku tatu yanalenga kuwajengea uwezo wajumbe wa Bodi katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, kuimarisha uongozi, usimamizi madhubuti, uwajibikaji pamoja na kuchochea utekelezaji wa mikakati ya mabadiliko yanayoendelea ndani ya TEMESA.
Mafunzo hayo yanaendeshwa na wawezeshaji kutoka Chuo cha Uongozi (Uongozi Institute), Dkt. Kassim Hussein, pamoja na Bw. Hussein Kakurwa kutoka Ofisi ya Msajili wa Hazina, ambao wanawajengea uwezo wajumbe wa Bodi kupitia maarifa na uzoefu katika maeneo mbalimbali ya uongozi na usimamizi.
Mafunzo haya ni sehemu ya jitihada za TEMESA za kuendelea kuimarisha uwezo wa viongozi na wajumbe wa Bodi ya Ushauri, ili kuhakikisha Wakala unaendelea kuwa na uongozi wenye uwezo wa kusimamia mabadiliko, kuleta ubunifu na kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake na utoaji wa huduma kwa wananchi.