KARAKANA YA TEMESA DAR ES SALAAM YAENDESHA KIKAO CHA WADAU

News Image

Posted On: August 13, 2021

Karakana ya Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mkoa wa Dar es Salaam leo imefanya kikao cha wadau kilichohusisha wadau wake wanaotumia huduma za Wakala huo ikiwemo wazabuni, taasisi za Umma, taasisi binafsi pamoja na washika dau mbalimbali ambao kwa namna moja au nyingine wanatumia huduma za Wakala huo. Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano hoteli ya Lamada Ilala jijini Dar es salaam, kimejadili mambo mbalimbali ikiwemo mapitio ya huduma za TEMESA kwa taasisi na idara za Serikali, dhana ya matengenezo ya magari, mikakati ya kuboresha huduma zitolewazo na kutokuzalisha madeni, pamoja na mada iliyohusu vipuri halisi na vyenye ubora (Genuine).

Lengo kuu la kikao hicho cha wadau lilikua ni kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili watumiaji wa huduma za Wakala, kupata ushauri wao , maoni na mwisho kuibuka na mkakati wa pamoja katika eneo la matengenezo ya magari