TEMESA YAENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA VIVUKO

News Image

Posted On: June 26, 2024

Lazaro Kilahala, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) akiwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji na Ujenzi wa Vivuko Eng. Sylvester Simfukwe, Tarehe 22 Juni, 2024, wamekagua miundombinu ya vivuko eneo la Bezi Wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza. Katika ziara hiyo pia, wamekagua maendeleo ya ujenzi wa maegesho ya kivuko upande wa Bukondo ambao unaendelea na mara ujenzi huo utakapokamilika, kivuko kipya cha Bwiro Bukondo ambacho kinaendelea kujengwa kikiwa kimefikia zaidi ya asilimia 85%, kinatarajiwa kuanza kutoa huduma katika eneo hilo.