MTENDAJI MKUU TEMESA AKUTANA NA WAZABUNI NA WASHITIRI KUJADILI MADENI
Posted On: May 19, 2026
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), Kheri Mahimbali tarehe Mei 18, 2026 amefanya kikao na wakandarasi na wazabuni wanaoihudumia TEMESA kutoka mikoa mbalimbali nchini wakati wa kikao cha pamoja kwenye Ukumbi wa Mikutano wa TEMESA Makao Makuu mjini Dodoma.
Katika mkutano huo, Bw. Mahimbali alipokea taarifa za madeni ambayo bado hajalipwa, pamoja na maoni na mapendekezo kutoka kwa wakandarasi na wazabuni. Alisisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana katika kuimarisha huduma za TEMESA ili kusaidia na kuharakisha maendeleo ya taifa.
Wakandarasi na wazabuni hao pia walimpongeza Mtendaji Mkuu wa TEMESA kwa kuteuliwa na kuahidi kufanya naye kazi kwa uwazi, uaminifu na uwajibikaji.