TEMESA YATINGA AAPM ARUSHA, KUONESHA HUDUMA BORA KWA KISHINDO
Posted On: May 14, 2026
Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) umeshiriki katika Mkutano Mkuu wa Pili wa mwaka wa Jumuiya ya Wataalamu wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Utumishi wa Umma (AAPM), mkutano huo ulifanyika katika viwanja vya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), jijini Arusha.
Katika mkutano huo, TEMESA ilipata fursa ya kuonesha na kutangaza huduma zake mbalimbali kupitia mabanda maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya wadhamini wanaoshiriki katika mkutano huo.
Ushiriki wa TEMESA ulilenga kuwafikia wadau wa taasisi za umma , pamoja na kutoa elimu kuhusu huduma za ufundi na umeme zinazotolewa na TEMESA, huku ikiimarisha ushirikiano na taasisi nyingine za Serikali.
Mkutano huo wa siku tatu ulifunguliwa rasmi tarehe 6 na mgeni rasmi Mhe. Ridhiwani Kikwete (Mb) Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.