TEMESA NA KARAKANA YA MAGARI ZANZIBAR ZATILIANA SAINI MAKUBALIANO YA MASHIRIKIANO
Posted On: November 21, 2023
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA) Ndg. Lazaro Kilahala na Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Karakana Kuu ya Magari Zanzibar (GAWS)Ndg. Hussein Abdi Hussein wakisaini hati ya makubaliano ya mashirikiano baina ya Wakala hizo mbili. Mashirikiano hayo yana lenga katika kujengea uwezo mafundi na yatawasaidia kupeana taarifa kuhusu matengenezo ya magari.
Utaratibu huo pia utawezesha wataalamu wa pande zote mbili kupata uelewa kuhusu vipuri feki na halisi vya magari kupitia kubadilishana uzoefu, wataalamu na taarifa.
Mkutano huo wa Mashauriano kati ya Serikali na Makandarasi na Washauri Elekezi wa ndani umefanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete ulioko mjini Dodoma na umejadili nafasi yao katika utekelezaji wa miradi na umeongozwa na Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa na Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba huku ukihudhuriwa pia na baadhi ya Viongozi akiwemo Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Daniel Chongolo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Rosemary Senyamule, Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Bara na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar.