WADAU WAOMBWA KUTOA MAONI YAO JUU YA UTOLEWAJI WA HUDUMA ZA TEMESA
Posted On: March 22, 2024
Mkurugenzi wa Huduma Saidizi Bi.Josephie Matiro amewaomba wadau wanaonufaika na huduma zitolewazo na TEMESA kutoa maoni yao ili waweze kufanya vizuri zaidi kufikia malengo.
Akizungumza katika mkutano wa kikao cha wadau kilichofanyika Mkoani Shinyanga Bi Josephine amesema kwa kipindi cha miaka miwili TEMESA imekuwa ikifanya marekebisho ya namna ya utolewaji wa huduma zake kwa wadau.
Amesema TEMESA imejitathmini na kufanya marekebisho upande wa karakana katika Mikoa 26 ili waweze kutoa huduma zilizo bora kwa wadau wake ikilinganishwa na mwanzo kwani kumekuwa kukiwa na malalamiko dhidi ya huduma zinazotolewa.
“Tunapita kuwasikia wadau wanasemaje kuhusu huduma zetu lakini pia kuwaeleza kile tunachokifanya na uwekezaji ambao unafanywa na serikali, kumekuwa na malalamiko mengi huko nyuma kuhusu TEMESA lakini tumejitathmini ,tumejipambanua na tumeanza kufanya marekebisho”.
Naye Mwakilishi wa Katibu Tawala, Bwa.Dedan Rutazika amewataka wadau kulipa kwa wakati huduma wanazozipata , ili TEMESA iweze kutoa huduma endelevu.
“Ukipeleka gari karakana unatarajia litengenezwe kwa viwango vikubwa na bei nafuu kwa hiyo kumbuka kulipa deni, kulipia huduma tunazozipata kwa harakaili tuweze kuendelea kupata huduma bora”amesisitiza.