HISTORIA FUPI YA UTOAJI WA HUDUMA YA VIVUKO KIGONGO BUSISI

News Image

Posted On: June 23, 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akieleza Historia fupi ya utoaji wa huduma ya kivuko katika eneo kati ya Kigongo Wilayani Misungwi na Busisi Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza. Rais Samia amefungua Daraja la J.P. MAGUFULI lenye urefu wa kilometa 3 na barabara unganishi kilometa 1.6 Juni 19, 2025.Daraja hilo linaunganisha Mikoa ya Kanda ya Ziwa na nchi jirani na litarahisisha usafiri na usafirishaji kwa Mikoa hiyo na nchi jirani.

Kutokana na kufunguliwa kwa daraja hilo, vivuko vitatu vya TEMESA, MV. MISUNGWI, MV. SENGEREMA na MV. MWANZA sasa vitahamishwa na kupelekwa maeneo mengine yenye uhitaji wa vivuko ili kuendelea kutoa huduma

HISTORIA YA KITUO CHA KIGONGO BUSISI

2.1 Mnamo:Mwaka 1968

Aidha kabla ya hapo kulikuwa vivuko vya watu binafsi vilivyo kuwa vikitoa huduma eneo hilo ambapo kivuko cha kwanza cha umma(serikali) kwa kuanzia mwaka 1968kilikuwa kinaitwa BUSISI BOAT. Uwezo wakeilikuwa ni kubebaAbiria 15 kilikuwa hakibebi magari kutokana na udogo wake.

2.2 Mnamo:Mwaka 1971

Serikali ilinunua kivuko kilicho fahamika kwa jina la MV MwanzaKilichokuwa na uwezo wa kubeba Tani 20sawa na magari madogo 3-4 kulingana na ukubwa,na Abiria 50 kivuko hicho kwa sasa ni Chakavu.

2.3 Mnamo:Mwaka 1972,

Serikali iliongeza kivuko kingine kilichojulikana kwa jina la Geita Feri. Kilikuwa na uwaezo wa Tani 65 ambayo kilikuwa na uwezo wakubeba magari 3 na abiria 100 ambacho kwa sasa kinafahamika kwa jina la MV TEMESA kinahudumia katika kituo cha ILUNDA na LUCHELELE mkoani Mwanza.Ambacho pia kilikuwa kinabebaTani 65magariMatano (5) Abiria 100.

2.4 Mnamo:Mwaka: 1977

Serikali ilinunua kivuko kingine amabacho kilifahamika kwa jina la MV Sabasabachenye uwezo wa Tani 85na kinabeba magari 10 madogo na 330na kwa sasa kipo kinaendelea na utoaji wa huduma kwa wananchi.

2.5 Mnamo:Mwaka 1985

Serikali ilinunua kivuko kingine kinachoitwa MV Sengeremaambacho niTani 170, kina beba magari 22 na abiria mia nne(400)na kwa sasa kipo kinaendelea na utoaji wa huduma kwa wananchi.

2.6 Mnamo:Mwaka 2008:

Serikali ilijenga kivuko kinachoitwa MV Misungwiambacho Tani 250uwezo wake ni kubeba Abiria 1000na magari kati ya 34 na 36na kwa sasa kipo kinaendelea na utoaji wa huduma kwa wananchi.

2.7 Mnamo:Mwaka 2018

Serikali ilijenga kivuko kinachoitwa Mv. Mwanza(Mwanza Hapa Kazi Tu)chenye uwezo wa kubeba Abiria 1000 na Magari 34 na kwa sasa kipo kinaendelea na utoaji wa huduma kwa wananchi.