WAWAKILISHI KUTOKA UNOPS WAFANYA ZIARA YA KIKAZI TEMESA MAKAO MAKUU
Posted On: February 28, 2025
Wawakilishi kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Huduma za Miradi, the United Nations Office for Project Services (UNOPS) leo wamefanya ziara rasmi ya kikazi katika ofisi za makao makuu ya Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA).
Wakati wa ziara hiyo, wamefanya mazungumzo na Menejimenti ya Wakala kuhusu usimamizi bora wa miradi mbalimbali inayotekelezwa na TEMESA kote nchini. Mada kuu zilizojadiliwa zilihusiana na miradi kama vile ujenzi wa vivuko, ununuzi wa vipuri vya magari, pamoja na vipuri vya mifumo ya umeme na elektroniki.
Masuala muhimu yaliyosisitizwa katika majadiliano hayo yalijikita katika majukumu ya UNOPS na TEMESA ya kutoa huduma bora za ununuzi na maendeleo ya miundombinu kwa wakati, kwa gharama nafuu, na kwa ubora wa hali ya juu. Juhudi hizi zinazingatia na kuchangia malengo ya Serikali ya Tanzania ya kufikia malengo ya maendeleo endelevu.